Sunday, November 16, 2008

Fat Joe na Eve - Funga Mwaka 2008















Mwanamuziki wa hip hop kotoka Unyamwezini Fat Joe na mwanadada mwingine machachari sana katika anga za kufoka foka aitwaye Eve na mwingine wa tatu (jina kapuni) watatua jijini Dar Desemba 8 kwa ajili ya kuangusha bonge la shoo.
Wadau funga mwaka huu mambo kama haya si ya kukosa kabisa, achana na suala la kuhadithiwa. ooh alifanya hivi,ooh alikuja na sijuiii niniiii aah haya maswali kama mtoto wa kijanja hupaswi kuuliza kiivyo, muhimu jichange mapema halafu tukajiachie au sio.
Sehemu ya kujiachia pamoja na kiingilio zitatajwa baadae, onyesho hili kubwa na la aina yake limeandaliwa na redio ya watu Clouds Fm,

Ricco bingwa Big Brother Africa 3 ,



















Ricco wa Angola ameibuka kuwa mshindi wa Shindano la Big Brother Africa III na kuibuka na kitita cha dola 100,000 (sawa za zaidi ya Sh milioni 100). Ushindi huo wa Ricco wa Jumapili iliyopita ulipatikana baada ya kupata kura ya nyongeza kutoka kwa Big Brother, Alexander Forbes, ambaye alimwongezea kura moja baada ya kura zake kulingana na mshiriki Hazel wa Malawi, huku mshiriki Munya akipata kura moja tu,

Odemba kupanda miti 20,000


















Mshindi wa pili wa shindano la Miss Earth ambaye pia alishinda taji la Miss Earth Air, Miriam Odemba, anatarajia kuanza kampeni ya upandaji miti elfu ishirini nchi nzima. Odemba alisema hayo jana baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Ufilipino alikohudhuria shindano la urembo la Miss Earth. Alisema anatarajia kuanza shughuli hizo baada ya wiki mbili zijazo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake kama Miss

T.I.D APEWA SIKU 10,









Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayetumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, Muhamed Khalid ‘TID’ ametakiwa kutoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama Kuu. Akitoa maelezo hayo jana, Dar es Salaam, Jaji wa Mahakama Kuu, Robert Makalamba alisema TID anatakiwa kutoa taarifa za kusudio lake hilo ndani ya siku 10 kuanzia jana na alimpa siku 45 kuandika ombi la kukata rufaa.

Muda wa awali aliotakiwa kukata rufaa wa siku kumi baada ya siku ya hukumu umepita. Lakini, wakili wa msanii huyo Masako Thomas, alisema kuwa Hakimu aliyemhukumu TID hakumweleza mteja wake kama alikuwa anaweza kukata rufaa ndani ya siku 10. Thomas aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama hiyo, kuwa hakimu huyo alikiuka sheria, kwa kuwa kisheria alitakiwa kumweleza hayo yote msanii huyo.

Katika hatua nyingine, kuliibuka mtafaruku kati ya baadhi ya wanahabari na kijana mmoja aliyekuwa akiwazuia kuingia ndani ya chumba ambacho kesi ilikuwa ikiendelea. Hata hivyo, ndugu wa karibu wa TID waliokuwapo mahakamani hapo waliwaambia waandishi kuwa hawana uhusiano na kijana huyo na pengine ni shabiki. Jaji Makalamba aliamuru TID arudishwe gerezani mpaka taratibu za rufani zitakapokamilika.

TID aliongozwa na maaskari kurudishwa gerezani ambapo akiwa njiani kurudi katika chumba cha mahabusu alisalimiana na mama yake mzazi na ndugu zake waliokuwa wamekaa nje wakisubiri yatakayojiri katika chuma cha mahakama. Julai 23 mwaka huu, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni, Hamisa Kalombola alimhukumu kijana huyo kwenda jela mwaka mmoja kufuatia kuridhika na mashahidi wote wanne na ushahidi walioutoa mahakamani kuwa TID alimpiga kichwani na mkononi kijana aliyefahamika kwa jina la Ben Mashibe.


Source: Habari Leo