Monday, February 29, 2016

Klex man ft Hard Mad - Queen ireen EATV

Monday, May 28, 2012

 Hon. Peter Msigwa writing has gone posed questions to some of them reketwa


  Hon. Leticia Nyerere (first picture left) in the launch of a branch of Chadema Washington Dc

 Hon. Nassari Joshua  (Dogo Janja) Akishanga hundreds of children who flocked to u DMV official launch branch of Chadema Washington Dc

Monday, October 3, 2011


Tarehe 10 ya mwezi Septemba, siku moja tu kabla ya Kumbukumbu ya Septemba 11, siku ambayo dunia nzima inakumbuka maadhimisho ya miaka 10 ya Septemba 11, Zanzibar ilipata Maafa ya kihistoria.

Jina langu ni SABRY, muathirika wa maafa ya kusikitisha ya MV Spice katika visiwa vya Zanzibar ambayo siku ya tarehe 9 Ijumaa ambapo meli hii, kwa kweli si meli ni Ferry tu ambayo imesajiliwa kubeba mizigo kutoka Zanzibar tu kwa sababu ya Usajili wake wa kazi katika Dare salaam, Tanzania ilikuwa imezuliwa na SUMATRA, Mamlaka ambayo inasimamia Usafiri wa Nchi Kavu na baharini Tanzania Bara kwa Sababu ya Hali Yake ya Usalam ana Kiufundi.

Nini kilichotokea. . . .? "Baada ya kuadhimisha kumalizika kwa Mwezi wa Ramadhani, Nilikuwa na ndoto mbaya juu ya familia yangu, na kwa sababu mke Wangu alipanga kusafiri, nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu safari hii." Alisema Sabry. 

Ni Utamaduni hapa Zanzibar kwamba, wakati familia inafunga ndoa ni lazima wanafamilia wote wa Familia wahudhurie na kutoa baraka kwa Bwana Harusi na bibi Harusi na kuwaaga. Kwa sababu ya mila hii nilitoa ruhusa kwa mke wangu kuhudhuria sherehe huko Matuuni Pemba, Kisiwa Cha Pili cha Zanzibar akiwa na Wifi Yake, Amina Mmanga na mtoto wake Mariam.

Nilifanya Maandalizi yote kwa ajili ya safari hii ikiwa ni pamoja na kuandamana naye mpaka Bandarini lakini sikuweza kupata fursa ya  kumpeleka hadi ndani kwa sababu hali ilikuwa mbaya kwani eneo la bandari kulikua na wasafiri wapatao 3,000 ambao wote wanataka kupanda ndani ya Meli hio. Nilimkabidhi mke wangu kwa Kaka yake ili amsaidie apande Ndani ya Boti, Sikujua kumbe Niliyakabidhi Maisha yake kwa Mungu.

Safari Iipoaanza . . . .
Meli ilianza Safari yake kutoka Dare salaam, siku ya Ijumaa tarehe 9 Lakini Ripoti zisizothibitishwa zinasema kuwa, meli ilikuwa imebeba mizigo na abiria zaidi ya uwezo wake na hii iliwafanya SUMATRA kuingilia kati na kuidhuia meli mpaka baadhi ya Mizigo iliposhushwa. Mabaharia Walishusha baadhi ya mizigo hadi SUMATRA waalipokubaliana na Hali hio na Kuruhusu Meli kuondoka.

MV Spice iliwasili Kisiwani Zanzibar siku hio hio jioni na abiria wapatao 300 (watoto wachanga na Wanaoingia bila ya Tiketi hawajahesabiwa) na ukadiriaji wa Abiria zaidi ya 100 ambawo hawakuwa katika Orodha ya meli. Moja ya tatu tu ya wasafiri kutoka Dare salaam walimaliza safari yao katika Bandari ya Zanzibar na inakadiriwa watu kati ya 200-250 walibaki ndani na Meli kwa Safari inayofuatiya, Safari ya Pemba.

Safari ya Pemba Ikaanza. 
MV Spice ilikuwa tayari na Wasafiri 350 na mizigo ambayo ni pamoja na chuma, Ngano, Mchele, Saruji na magari, inakadiriwa Mzigo tu ulikua Tani 500!. 

Usalama wala Meli mara nyingi unaweza kuathiriwa na hali ya hewa mbaya , Bahari Chafu, Kugongana na Chombo chengine au miamba. Aidha, kanuni za Bahari zinataka Nahodha na Baharia kulinda usalama wa Abiria wao ikiwemo kufuata kanuni zote za usafiri wa Baharini kama Kujaza kwa Idadi na Kuwa na Makoti ya Kuogelea kutokana na Namba ya abiria waliochukua ama zaidi.

Katika Mamlaka ya Bandari Zanzibar Meli iliruhusiwa kubeba watu 610 ambao walikua Wasafiri Wapya kwa mujibu wa Orodha ya meli ikiwa ni pamoja na watoto zaidi ya 400 ambawo hawakuonyeshwa katika Orodha ya Meli sababu waliruhusiwa kupanda meli bila tiketi. Tunasema zaidi ya watoto 400 kwa sababu ni Mila na Silka hapa Zanzibar kwa watoto kusafiri na kwenda kula Sikukuu ya Eid na Familia zao maana Shule pia huwa zimefungwa kwa Kipindi kirefu. Pia kuna idadi ya Abiria wengi ambao hawakukata Tiketi walipigwa Mihuri Mikononi na Idadi yao haijulikani.

Hivyo jumla ya idadi ya wasafiri waliopanda Boti hii Inakadiriwa kuwa kati ya 1500 – 2500.

Wakati wa kuondoka Bandarini Zanzibar kuna baadhi ya Abiria wametoa Ushuhuda kua walipoona Meli imejaa sana walishuka na Jamaa zao lakini Mabaharia walipoona hivyo kwa tamaa ya Biashara waliwazuia wasitoke wengine wanasema waliwazuia wasitoke maana ingeanzisha vurugu na Meli ilikua imeshaanza kuyumba wakati bado ipo Bandarini! .Pia walipoanza kuiondoa Meli ilianza kuyumba na wakaamua kuirudisha tena Bandarini na Kuitazama Tatizo Kisha walipoona haiyumbi tena, Haoooo wakaanza Safari ya Pemba.Kawaida inachukua masaa Nane Mpaka Kumi Kufika Pemba.Kuna Ripoti zisizothibitishwa kua hata Mmiliki wa Meli aliaambiwa kuhusu hatari kama Nahodha angeondoa Meli, ila baada ya kushauriana na Wenzako Wakasema, "Haya Ombeni Mungu" na Safari ikaanza,Kilisema Chanzo hiki cha Habari.

Haya, Na Safari ya Pemba Ikaanza . . . . . .

"Ilikuwa karibu na usiku wa manane wakati nilipopokea simu kutoka kwa Shemegi Yangu, Dada wa Mke wangu Akisema,Sabri Jikaze Kaka angu, kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa kwamba MV Spice Islander inazama! Hamadi ! Nilishtuka sana na Taarifa hizi na kutokana na Hali ya Wasiwasi niliyokua nayo kabla mke wangu hajasafiri niliziamini Taarifa hizi na Kuanza Kumuombea Mke wangu "! Alisema Sabry 

Sabry akaendelea, Nilikuja Kujua Baadae kuwa Mke wangu alimpigia Simu Dada ake na Kumwambia “ Mpaka sasa Meli inazama na Dada tusameheane, Mwambie Shemegi Yako tusameheane na muniombee dua mi natangulia nawasubiri Akhera . . . .  Simu ikakatika dalii za Kuishiwa Chaji.” Alimazia Sabry

Mamlaka za Zanzibar zina Nini la kusemaaaaa ... ..
Mpaka sasa Ripoti za Serikali ya Zanzibar zinasema Abiria waliosajiliwa na meli hio ni 610 Lakini cha Kujiuliza, Ni hao hao waliotangaza watu waliookolewa ni 619 na Maiti zilizopatikana ni 202, Je, Wanajua Hesabu vizuri hawa!

Baada ya Juhudi binafsi ya Wabunge, Hadi sasa watu wafuatao hawajulikani Walipo, Kojani (108) Ole (157) Micheweni (88) Magogoni (184) Wete (149) Gando (418) Mtambwe (214) na Konde (96)Jumla watu ambao inaaminika waliku katika meli hii na hawajapatikana ni 1,596,Sasa tukijumlisha na Maiti (202) na waliookolewa (619) Jumla ya watu waliokuemo ni (2,214) Kwenye Meli iliyosajiliwa Kuchukua Mizigo na abiria wachache.

Kwenye mahojiano rasmi na Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC), Muheshimiwa Hamad Masoud (Engineer) Waziri wa Usafiri Zanzibar alisema kuwa, kati ya sababu ya ajali hii ni kwamba Wazanzibari wana mila ya kusafiri kwa makundi na Kifamilia, watoto wengi, na wanaweza kupanda melini hata kama itajaa vipi, Alisisitiza kuwa Serikali ina sehemu yake ya kuhakikisha Ajali kama hii kamwe haitokei tena.

Sasa Mamlaka zitujibu Masuala yafuatayo

1. Mara nyingi Mamlaka za Zanzibar zimeweza Kuzuia Mandamano ya Kupinga Serikali, Wanafunzi au Mikusanyiko ya Dini, Imeshindwaje kuzuia Meli hii isiondoke, Au Walikua washalala?

2. Muda Mfupi uliopiopita kuna Ajali ya meli iliwahi kutokea ya MV Fatihi ambayo kwa Uzembe ilizama Wakati imeshafika Bandarini ikitokea Daresalaam, Japo kuna watu waliwahi Kushuka lakini Baadhi hawakuwahi na kufa Maji.Tume ikaundwa na Jambo Moja ililoligundua ni kwamba Meli zinapakia sana Mizigo na Watu, Mbovu sana na hazina Vifaa vya kutosha wakati wa dharura na Serikali ikawahakikishia wananchi kua Ajali kama hii haitoweza kutokea tena, Baada ya Ajali hii, Je Serikali inasemaje?

3.Kabla Meli haijaanza safari Maafisa wa Bandari, kabla hawajairuhusu meli kuondoka ni wajibu wao kuangalia utabiri wa hali ya hewa; kama kuna Maboya ya kutosha katika kila kiti na sehemu za wazi hasa za Milangoni za Meli , Mstari wa kuonesha Alama ya Kuelea kwa Meli upo katika kipimo Sahihi kuonesha kua hakuna dalili ya uzito ulipotiliza.Je haya yote yalizingwatiwa?

Baadhi ya Ripoti zinasema, Bado Kuna maiti wengi kwenye Melii hii Ambayo imezama Takribani Mita 350 Chini ya Bahari kiasi ya kufanya Mabingwa wa kijeshi wa Kuzamia kutoka Afrika kusini kushindwa kuifikia maana Vyombo vyao vya kisasa vinawawezesha kuzama Mita 50 tu chini  ya Bahari.Kama wazungu wameshindwa wataweza Wabongo!

Mengi yanasemwa na yatasemwa kua, Kama hamu yao ilikua ni Kutengeneza TITANIC ya ZANZIBAR, Wamefanikiwa.Na wajiandae kwenda HOLLYWOOD Kuchukua Mshindi wa Filamu za Baharini.

Ushuhuda
"Nilikuwa katika MV Spice Islander na tulipofika Nungwi meli ilipasuka na kuanza kuingiza Maji Upande Mmoja, Mabahari walitunadia kuelekea Upande wa Pili ambao nao ulikati na Maji yakaanza Kuingia.Taharuki ikaanza na Mabaharia Wakatangaza Hali ya Hatari kila mtu ajiokoe,tukatupiwa magodoro Mapya Baharini na wengine wakavaa makoti ya kuogolea na tukapiga Mbizi (Tukajitupa Baharini) "alisema mmoja wa wasafiri

"Niliona idadi ya maiti wengi pwani ya Nungwi" Kilisema Chanzo chengine cha Habari.
“Hakika sote tumeumbwa na Mungu, Na Hakika sote kwake tutarejea, tutake tusitake”Alimaliza Sabry kwa Majonzi

Monday, June 13, 2011

                                                        NAINGIA TENA   DENMARI <="" tena ="">
                                       MPAKANI MWA UJERUMANI NA UHOLANZI



SOLAR PANEL ROOF  KAMA BONGO TUKIJENGA HIVI  ATUWEZI KUWA NA GIZA TENA



                       WIND FARM  KAMA UNAVYO ONA MDAU HIZI ZIPO UJERUMANI 

Wednesday, June 8, 2011






                                          NIPASHE
Ukitaka kuona sura halisi za wabunge wa Tanzania gusa posho zao, huo ndio msimamo wao wa miaka na miaka na jana ulijidhihirisha kufuatia ushauri wa Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe, wa kutaka kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge katika bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012.
Jana baadhi ya wabunge hasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), walipinga kwa nguvu zao zote mapendekezo ya Zitto ya kutaka posho za vikao wanazolipwa ziondolewe.
Wa kwanza kupinga mapendekezo hayo bila hata kutafuna maneno alikuwa ni Mbunge wa Manyoni Mashariki (CCM), John Chiligati, ambaye alisema kama wabunge wa kambi ya upinzani hawataki kuzipokea fedha hizo waziache.
Chiligati alitoa msimamo huo jana jijini Dar es Salaam, alipotakiwa kutoa maoni yake kama anaona kuna haja posho za wabunge kuondolewa kama ilivyopendekezwa na Naibu kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Zitto Kabwe.
Akizungumza na NIPASHE katika viwanja vya ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, Chiligati ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), alisema hoja hiyo sio ya wabunge wote bali ya upinzani na hivyo kama wao wanaona hawazihitaji posho hizo wasizichukue.
“Hii kambi ya upinzani kama haitaki hailazimishwi kupokea posho hizo za vikao wanaweza kuziacha sio lazima wazipokee,” alisema.
Naye Mbunge wa Magomeni visiwani Zanzibar, Mohammad Chomboh (CCM), alisema suala hilo halitekeleziki kwa kuwa Sh. 80,000 anayolipwa mbunge kama posho ni ndogo ikilinganishwa na hali halisi ya maisha ilivyo sasa.
Alisema kulala nyumba ya wageni kwa siku wanapokuwa Dodoma ni Sh. 50,000 hapo bado hawajala hivyo kiasi hicho sio kikubwa kama inavyoelezwa na upinzani.
Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza (CCM), alisema hoja ya kutaka posho ifutwe ni mawazo ya mtu kwani waliopanga malipo ya posho hiyo nao pia wana sababu zao.
Hata hivyo, alimtaka mbunge yeyote mwenye hoja kama hiyo, aipeleke bungeni ikajadiliwe huko, badala ya kuizungumzia nje ya Bunge.
Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Hamisi Kigwangalla, alisema haungi mkono hoja ya Zitto, kwa vile imejaa unafiki na kujitafutia umaarufu.
“Kama kweli tuna dhamira ya msingi ya kutumikia Watanzania kuna vitu vingi vilipaswa viondolewe na si posho peke yake. Kwa mfano, mashangingi yangefutwa kwa sababu yana gharama kubwa kuendesha.
Lakini yanahitajika kwa wabunge kutumia kuwafikia wananchi vijijini,” alisema Dk. Kigwangalla.
Alisema posho za vikao, ambazo Zitto anataka zifutwe, ni ndogo kulinganisha na majukumu yanayomkabili mbunge.
Dk. Kigwangalla alisema hata shida binafsi za wananchi, wanategemea zitatuliwe na mbunge, hivyo ni vigumu mbunge kufanya kazi bila kulipwa posho.
“Vinginevyo wanataka mbunge arudi mitaani kuganga njaa. Kwa hiyo, hiyo ni kauli ya unafiki, ya wanasiasa wanaotafuta umaarufu, mimi siwezi kuiunga mkono,” alisema Dk. Kigwangalla.
Kwa sasa mbunge analipwa Sh. 70,000 kwa siku kwa ajili ya kujikimu pamoja na Sh. 80,000 kama posho ya kikao kwa siku ambapo jumla analipwa Sh. 150,000 mbali na mshahara wake.
Kwa upande wake, mbunge wa viti maalum (CCM), Dk. Maua Daftari alipoulizwa kuhusu hoja hiyo hakuwa na jibu la kutoa.
Badala yake mbunge huyo alibaki anaguna na kukata simu bila ya kuiunga mkono ama kuikataa hoja hiyo.
Akitoa maoni yake, Ali Khamis Seif mbunge wa jimbo la Mkoani (CUF), alisema hoja ya kutaka posho ziondolewe ni nzuri lakini kwa sasa bado sio wakati wake.
Alisema mbunge ana kazi nyingi za kuwasaidia wananchi hivyo ikiwa ataondolewa posho watashindwa kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Hata hivyo alisema ikiwa fedha hizo zitaondolewa kwa mbunge ziingizwe kwenye mfuko wa jimbo ili zisaidie kusukuma mbele maendeleo ya wananchi.
Alitoa mfano kuwa kuna wabunge wengine wanatumia fedha hizo kuwasaidia wapiga kura wao kupata elimu pamoja na kupata matibabu kazi ambayo ingepaswa kufanywa na serikali.
Akizungumzia hoja hiyo, mbunge wa viti maalum (CCM), Diana Chilolo, alisema Zitto ana mtazamo finyu juu ya hoja hiyo ya kutaka posho ya vikao iondolewe. Alisema fedha anayoipata mbunge sio ya kwake pekee bali inawasaidia wananchi wengine wakiwemo yatima, walemavu, wajane katika kupata mahitaji yao.
Kila anapokuwa mbunge wananchi wake wanamuona kama nguzo na kimbilio lao, hivyo posho hizo zinasaidia kutatua matatizo madogo madogo kama hayo.
Mbunge wa jimbo la Meatu (Chadema), Meshack Opulukwa, akitoa maoni yake alisema bado anatafakari hoja hiyo.
Aliongeza kuwa hoja hiyo aliisikia jana, lakini kama Waziri Kivuli wa Kilimo, Chakula na Ushirika bado anaitafakari ili kuona kama ataiunga mkono hoja hiyo itakapopelekwa bungeni.
Mbunge wa Muhambwe (NCCR-Mageuzi), Felix Mkosamali, aliunga mkono hoja ya Zitto ya kutaka wabunge wasiwe wanalipwa posho za vikao.
Mkosamali alisema si posho tu, bali anataka pia mishahara wanayolipwa wabunge pia ipungue na kuwa chini ya ile wanayolipwa hivi sasa kwani hatua hiyo itasaidia kudhibiti mafisadi kuwania ubunge.
“Hatuhitaji watu wagombee kwa ajili ya kupata posho, maana kuna watu huwa wanagombea kwa lengo la kutafuta maslahi binafsi na si kuwawakilisha Watanzania, hivyo posho ikiondolewa na mishahara ikapunguzwa waroho wa madaraka watapungua” alisema Mkosamali.
Aliongeza: “Kwa hiyo, naunga mkono hoja ya kufutwa posho. Lakini mishahara ya wabunge pia ipungue, maana haiwezekani posho zipungue wakati mishahara iko palepale,” alisema. Mkosamali alisema kufutwa kwa posho kwa wabunge ni hatua muhimu kwani kuna maeneo mengi ya kijamii, kama vile hospitali, fedha hizo zinaweza kupelekwa kusaidia.
Alisema pia kupunguzwa kwa mishahara ya wabunge, ni muhimu kwani kutasaidia kuwafanya wanaotaka kuwania ubunge, kufanya hivyo kwa lengo la kuwawakilisha wananchi kwa dhati.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, naye pia aliunga mkono kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge, lakini alishauri posho hizo zibaki kwa vikao vya watumishi wasio na mishahara, kama vile wenyeviti wa vijiji.
“Mtumishi yeyote alipwe posho ya vikao, ambavyo sio sehemu ya majukumu yake,” alisema Kafulila.
Hata hivyo, alisema malipo ya posho za vikao, yasiishie tu kufutwa kwa wabunge, bali yafutwe serikalini na kwenye mahakama pia.
“Hatupaswi kulipwa kwa kukaa. Pesa nyingi inavuja. Mfumo wa sitting allowance (posho za vikao) must end (ikomeshwe),” alisema Kafulila.
Alisema pia posho nyingine zote zinapaswa kutozwa kodi na suala hilo liwe ni utaratibu na sera kwa mihimili yote ya dola; Bunge, Serikali na Mahakama.
Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu, aliunga mkono si kufutwa tu kwa posho za vikao kwa wabunge, bali hata mishahara nayo pia ifutwe akisema kazi ya ubunge haitakiwi malipo.
“Mimi maoni yangu ni kwamba, kwa kazi ya ubunge, wabunge hawapaswi kabisa kulipwa hata mshahara, ikifanyika hivyo itawafanya watu kujikita zaidi katika kuwatumikia wananchi,” alisema Mangungu.
Kwa upande wake, mbunge wa Mpanda mjini (Chadema), Said Arf aliunga mkono hoja hiyo ya Zitto na kusema kuwa umefika wakati wabunge kuwajali wananchi wenzao kwa kukubali kuachia posho zao ili ziweze kuwasaidia.
Aliwataka viongozi kupunguza anasa ili fedha hizo zisaidie watu wenye mahitaji ya lazima ikiwemo kuwapatia maendeleo.
Alisema mfumo unaotumiwa na Bunge wa kusema “ndiyoooo au hapanaaa” katika kupitisha hoja mbalimbali haufai kwa kuwa huo ni mfumo wa kijima.
Aliongeza kuwa hoja hiyo ya kutaka posho hizo ziondolewe inaweza kukwamishwa kwa kutumia mfumo huo wa upigaji kura kwa kusema ndiyo au hapana.
Juzi Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema haoni sababu mbunge kuendelea kulipwa posho nono kwa ajili ya kuhudhuria vikao kwa kuwa hiyo ni sehemu ya kazi yao ya kila siku.
Alisema anataka sheria ya Bunge inayotoa mwanya kwa wabunge kulipwa posho hizo ibadilishwe haraka ili kiasi hicho cha fedha kitumike kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania wengine wenye matatizo.
Zitto alisema ingawa suala hilo ni gumu, lakini ataliwasilisha katika mkutano wa Bunge la bajeti wakati atakapowasilisha bajeti yake kama Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi.
Alisema ana imani wabunge wenzake watakubali pendekezo hilo na kumuunga mkono kubadilisha sheria hiyo ili posho hizo zisiwe zinatolewa.
Katika Bunge lililopita aliyekuwa Mbunge wa Karatu, Dk. Willibroad Slaa (Chadema), aliwahi kutoa wazo kama hilo pamoja na kupendekeza mshahara wa wabunge upunguzwe kwa kuwa ni mkubwa, lakini wabunge wenzake walipinga hoja hiyo kwa nguvu zote.
Dk. Slaa alishindwa kupitisha hoja yake katika Bunge lililopita baada ya wenzake kukataa kumuunga mkono huku baadhi yao wakitoa kauli za kumkejeli na kumuona kama mtu aliyekuwa akitafuta umaarufu wa kisiasa. Kiutaratibu wabunge wote hulipwa posho ya vikao ya Sh. 80,000 kwa siku, na posho ya kujikimu kwa kuwa nje makazi ya Sh. 70,000 hivyo kwa siku moja tu wabunge hulipwa wastani wa Sh. 150,000 siku za kazi, wakati mwishoni mwa wiki hulipwa Sh. 70,000, kwa maana hiyo kati ya wabunge wote waliopo ambao ni 350 kama posho hizo zitaondolewa serikali itaokoa kiasi cha Sh. milioni 52.5 kwa siku.
Mkutano wa Bunge la Bajeti unatarajiwa kuanza Juni 7, mwaka huu hadi Agosti 15, mwaka huu, kwa maana hiyo kutakuwa na siku za kazi 48 ambazo zitaigharimu serikali Sh. bilioni 2.52 kama posho ya vikao kwa wabunge.
Kiasi hicho kikiongozewa Sh. milioni 490 za posho ya kujikimu ya mwishoni mwa wiki ambazo ni kwa siku 20, serikali itakuwa inaokoa jumla Sh. bilioni 3.01 ambazo ni posho za wabunge bila mshahara.
Kiasi hicho kinaweza kuelekezwa kutunisha bajeti ya elimu, barabara au afya, ambako kuna upungufu mkubwa wa fedha.
Mshahara wa mbunge kwa sasa ni Sh. milioni 2.5, kiasi hicho kikichanganywa na posho ya mafuta, kuendesha ofisi mapato yake ya ubunge yanafika kiasi cha Sh. milioni 7.19.
Serikali inatarajia kutumia Sh. trilioni 12.8 kwa mwaka wa fedha wa 2011/2012, kati ya hizo Sh. trilioni 8.8 ni kwa matumizi ya kawaida, yaani posho na mishahara na ulaji mwingine, wakati fungu la maendeleo ni Sh. trilioni nne tu.
Utaratibu wa kupitisha bajeti ya ulaji umekuwa ni utamaduni wa taifa hili, kwani hata mwaka huu wa fedha unaomalizika serikali ilipitisha bajeti ya Sh. trilioni 11.6, kati yake Sh. trilioni 7.7 zilikuwa kwa fungu la kawaida na Sh. trilioni 3.8 kwa ajili ya maendeleo.
Soma maoni yetu ukurasa wa sita
CHANZO: NIPASHE