Tuesday, January 27, 2009

Makasi: Ivory Coast njia ya kwenda Ulaya















Profesa Jay: Wanaoua albino ni hatari kuliko mafisadi wa EPA na Richmond,

MSANII mkongwe wa miondoko ya hip hop nchini, Profesa Jay ametangaza kuuanza mwaka 2009 kwa kuingia kwenye vita dhidi ya mauaji ya Watanzania wenye ulemavu wa ngozi Albino?

Profesa Jay ambaye jina lake halisi ni Joseph Haule ameiambia Mwanaspoti kwamba, pamoja na ukatili huo kuonekana ni kama filamu au hadithi kwa watu wengine hapa nchini.


Anaamini Tanzania imekuwa ikiingia katika aibu kubwa kimataifa kutokana na suala hilo na kupoteza sifa ya Tanzania kwamba ni nchi ya amani.


?Wako ambao wanaamini hakuna Mtanzania leo anaweza kushika kisu akadhubutu hata kumchoma mwenzake, yote hiyo kwa kuwa wanajua sifa ya nchi hii kuwa ni ya amani. Sasa leo inawezekana vipi kuwepo na watu ambao wanaua watu kwa kuwakata viungo wakiwa hai.


?Mimi siamini kama kuna mtu anajaribu kufumba macho na kujaribu kuyafikiria maumivu ambayo wanapata Watanzania wenzetu ambao wanaishi maisha ya kukimbia na kubahatisha kama vile ni wahalifu tena hatari.


Unaamka asubuhi unaona kwenye BBC na CNN eti Tanzania inajadiliwa kwa suala hilo, tena ni nchi pekee duniani.


?Sidhani kama serikali imetumia nguvu zake zote kupambana na hili suala kama ilivyofanya kwa mengine. Kuna adhabu ya kifo, hiyo ndio inastahili kuwa ya wale watakaopatikana na hatia kwa kuwaua Albino, huu ni ukatili wa hali ya juu.


?Najua nchi kadhaa zimekuwa zikipiga vita adhabu ya kifo, lakini leo angalia katika hali hiyo unafikiri mtu wa namna hiyo anastahili adhabu nyingine ipi.


Tumeelezwa kwamba wahusika wakuu ni vigogo na wengine wako serikalini. Naamini kabisa inawezekana kuwatia nguvuni na inaonyesha kwamba ugumu wa mambo unatokana na wengi kuwa na uwezo mkubwa wa kifedha.


?Tunajua kuna viongozi wana imani za kishirikina na hili ndio tatizo la mauaji ya Albino, kama tunasikia mkono tu wa Albino unaweza kuuzwa kwa zaidi ya Sh milioni 10 hauoni hizi ni dalili kwamba suala hili linahusika sana watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha.


Watakuwa kina nani zaidi ya vigogo?* anahoji Profezsa Jay. *Nadhubutu kusema suala hili ni hatari na linakiuka haki za binadamu kupindukia, hauwezi hata kuliringanisha na sakata la EPA na Richmond.

Wauaji tuko nao, sababu ipi inafanya tusiwapate na kuwatia nguvuni na kumaliza hili.? Anaendelea, ?Mimi nitatoa mchango wangu, nimesikia wasanii kadhaa wameimba kuhusu suala hili, hivi karibuni nitaingia studio kuimba kuhusu hilo nitasisitiza vita kubwa dhidi ya hili.


Sitasita kuimba kwa kuwa wengine wameshafanya hivyo kwa kuwa najua mapokeo ya sauti ya kila msanii kwa mashabiki ni tofauti, huu utakuwa ni mchango wangu,? anasema.


Akizungumzia kuhusu suala la matayarisho na mpangilio wa kazi zake kwa mwaka 2009, Profesa Jay alisema hip hop ina heshima kubwa tofauti na inavyochukuliwa hapa nyumbani na anataka kubaki msitari wa mbele kuwaongoza wasanii wengine kulinda na kuiendeleza heshima.


?Kingine ni kupata sapoti kutoka serikalini na mashabiki wenyewe ambao siku zote ninasema kuwa wao ndio wenye muziki. Kama ninaimba kwa ajili ya watu fulani basi ni mashabiki wangu, wasiponiunga mkono wao nani atafanya hivyo?


?Nilikuwa Nigeria katika tuzo za MTV, zilifanyika Novemba 22, 2008 katika mji wa Abuja. Huwezi kuamini ni tuzo tatu kati ya zaidi ya 20 ndio zilitoka nje ya Nigeria kwa kuwa mashabiki wao waliungana na kuwapigia kura wasanii wao hadi wakawazidi hata Wamarekani na kuzitwaa zote, huo ni mfano na chamgamoto kwa mashabiki wa hapa nyumbani na wanatakiwa kuiga.


?Hakuna haja ya kusema wewe ni shabiki wa Profesa Jay, kama Jaydee au Mwana FA ameingia kwenye kinyang ?anyiro cha kimataifa basi huo ni Utanzania. Tunamuunga mkono kwa pamoja, katika MTV nilikuwa nawania tuzo ya msanii bora wa hip hop nikichuana na wasanii wawili wa Marekani, Lil Wayne na The Game, pia Mnigeria Nice aliyeshinda na Msauzi, HHP.


?Wanigeria hadi mawaziri walipiga kampeni wasanii wao waungwe mkono na mashabiki lakini hapa nyumbani niliondoka kama yatima ingawa nilikuwa anaenda kuliwakilisha taifa nikichuano na watu wa mataifa makubwa. Utaona Mamis wakiwa wanaenda kushiriki mashindano wanakabidhiwa bendera, vipi wasanii mbona haiwi hivyo. Kuna haja ya mabadiliko kadhaa yafanyike na serikali iingie huku na kusaidia,? anasema Profesa Jay akisisitiza kwa mikono.



Profesa Jay aliyeibuka msanii bora wa kiume wa Tanzania katika tuzo za PAM za Uganda huku Jaydee akiwa bora wa kike anaisisitiza kwamba changamoto kwa serikali na mashabiki kuwaunga mkono wasanii.


Hata hivyo anasisitiza kwa wasanii wenzake, ?Wako wale ambao wanavimba kichwa kwa mafanikio kidogo tu, wajue wanapaswa kukubali kukosolewa ili tuweze kupiga hatua. Sisi ni binadamu, hatuwezi kuwa tunajua kila kitu. Kama unakataa kukosolewa leo, kesho wewe utawakosoa vipi wengine.?


?Lakini pia wakati mashaniki wanatuunga mkono basi wasiangelie jina la mtu au umaarufu wake, waangalie kazi na kumpa moyo yule anayefanya vema kwa kuwa inakuwa ni kwa ajili ya maendeleo ya muziki wa Tanzania,? anasema Profesa Jay maarufu kama Heavy Weight MC.


Profesa Jay alianza kuchipukia kimuziki mwishoni mwa miaka ya 1990 akiwa na kundi la Hard Blasters (HBC) akiwa na Willy na Terry na walifanikiwa kushinda ubingwa wa kundi bora la hip hop kabla ya kuweka rekodi ya kuwa kundi la kwanza la miondoko hiyo kufanya maonyesho mikoani wakitumbuiza.



















Na Saleh Ally
UKISEMA ni suala linaloumiza vichwa vya mashabiki na wadau wa muziki wa kizazi kipya sawa kabisa, ukiongeza kuwa inakatisha tamaa pia ni sawa ila hali halisi ni kwamba kundi la TMK Wanaume Family limemeguka kwa mara ya pili na kusababisha kuzaliwa kundi jingine la tatu kutoka ubavuni mwake.

Kundi la Wanaume TMK Family lililozaliwa mwaka 2004 jijini Mwanza, lilikuwa ndio kundi linaoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi zaidi katika muziki wa kizazi kipya kabla kukumbwa na matatizo ya kujiengua kwa wasanii wake zaidi ya watano wakiongozwa na Juma Nature walioanzisha kundi jingine la Wanaume Halisi.

Meneja wa Wanaume TMK Family, Said Fella alionyesha ujasiri mkubwa kuliongoza kundi bila ya kuyumba na kufanikiwa kuendelea kufanya vema na kutoa ushindani mkubwa.

Baada ya miezi kadhaa, kundi hilo limemeguka tena baada ya wasanii wake watatu, YP , Y-Dsh na Jenebi Mbaraka �Jebby� kuamua kujiengua na kuunda kundi jipya la Temeke Unit.

Hali hiyo imesababisha kuibuka kwa maswali mengi miongoni mwa wadau wa muziki huo na kuanza kujiuliza kulikoni, je, Fela anaweza kuwa ni tatizo kubwa hadi vijana hao kuchukua uamuzi wa kusambaa kila baada ya miezi kadhaa. Lakini kuna wengine kama Mheshimiwa Temba, KR Mullah na Chegge wameendelea kudumu chini ya uongozi wa meneja huyo, tatizo ni lipi hasa?

Jebby, ambaye ameanzisha Temeke Unit akiwa na YP na Y-Dsh, pacha walioanza kujulikana baada ya juhudi kubwa za Fela kuinua vipaji vyao ameiambia Mwanaspoti kwamba kilichowandoa ndani ya Wanaume Family si ugomvi binafsi na badala yake ni suala la maslahi.

"Hakuna mwenye ugomvi binafsi na mtu, suala kubwa hapa ni maslahi. Fela ni mtu aliyesababisha kuibuka kwa makundi ndani ya kundi kutokana na kuwapendelea baadhi kwa kiasi kikubwa huku wengine wakionekana hawana kitu.

"Lakini kitu cha ajabu, wanajumuika katika kufanya shoo, malipo makubwa yanakwenda kwa Temba, Chegge na KR. Haikuwa hali nzuri kwa kuwa nakumbuka shoo moja ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaamm, Y Dash na Temba walikunjana na kutaka kupigana. Suala lilikuwa hilo hilo la maslahi.

"Katika shilingi milioni moja, walitaka wengine wagawane laki tatu tu wakati saba iende kwa wachache. Ilikuwa tafrani lakini ikaishia kwa kuwa na mabadiliko hata kidogo kwa watu kupata angalau kiwango cha juu kidogo," anasema Jebby, ambaye ndiye kiongozi wa kundi la Temeke Unit au TMK Unit.

Tayari kundi hilo limeipua singo ya ?More Fire? iliyorekodiwa jijini Kigali, Rwanda mwezi uliopita kwa kushirikiana na wasanii wa nchini humo Sister Mimi na Back T.

Singo hiyo ni maandalizi ya albamu ya kwanza ya TMK Unit itakayojulikana kwa jina la 'Kidonge' na Jebby anasema wana imani hadi mwezi Aprili itakuwa imeingia sokoni, tayari kwa walaji. Licha ya albamu, wamepanga kuzindua mavazi yao chini ya Chilu Latest Wear, maandalizi yanafanyika nchini China.

Pamoja na yote, Jebby anasema inaonekana Fela amechukizwa na kitendo cha wao kujitoa na ameanza kutuma ujumbe mfupi wa simu wenye vitisho.

"Amenitumia, anaonekana kuchukizwa na kutoa vitisho. Kwa kweli inashangaza kwa kuwa mimi binafasi sina ugomvi naye lakini nisingependa kudhulumiwa kimaslahi halafu nikae kimya kwa sababu ya nidhamu," anasema.

Mwanaspoti ilimsaka Fela, juzi Jumapili naye alikiri kwamba ni kweli alilazimika kuwalipa fedha nyingi zaidi akina Temba, Chegge na KR kwa kuwa ndio vipenzi vya mashabiki wa kundi hilo.

"Kweli nimechoka sana, wote hao (Jebby, YP na Y Dash) walikuja mikono nyuma. Walionyesha kuwa na nidhamu ya juu huku kila mmoja akitoa sababu kibao, kwamba ana shida sana na pamoja na muziki anahitaji msaada.

"Nakupa mfano wa gereji, msaidizi hata siku moja hawezi kulipwa sawa na fundi mwenyewe. Sasa inakuwaje nimlipe Y Dash sawa na Temba kweli inaingia akilini. Hata wewe ungekuwa ni kiongozi sidhani kama ungefanya hivyo.

"Naweza kusema kilichotugombanisha ni kitu cha kijinga, kuna gazeti liliwahi kuandika kwamba kuna msanii mwenzetu amelawitiwa baada ya kulewa chakari. Tulimuita msanii huyo kwenye kikao cha kundi na baada ya kufuatilia tuliona ana hatia ya utovu wa nidhamu, tukamsimamisha.

"Baada ya hapo, Y Dash akaibuka na kuanza kumsaidia huku akionyesha dharau za wazi kwa KR eti kwamba hana lolote katika mchango wa kundi. Mara kadhaa alikwaruzana na Temba, ambaye alitaka suala la heshima lichukue mkondo, KR kaanza muziki mwaka 1992. Leo ni kama nguzo ya kundi, vipi mtu kama Y Dash aonyeshe dharau wazi wazi namna ile," alihoji Fela na kuongeza.

"Kila mtu atazungumza lake, ila mimi roho inaniuma sana, Y Dash nilimtoa mitaani wakati YP alikuwa mcheza shoo kule Keko. Mimi ndiye niliwachukua na kuwaunganisha hata leo wanaishi maisha ya nafuu. Nilikuwa kama baba wa Y Dash, ambaye sasa ni yatima, dharau yao inaniumiza sana.

"Angalia, wakati wanakwenda Rwanda tuliwasiliana, walipokuwa huko walinipigia. Wamerudi wamechukua uamuzi huo na kuanza kunipaka matope.

"Nimechoka kwa kweli, kila anayekuja na hali mbaya ya maisha akiwa mikono nyuma na heshima nyingi. Akipata mafanikio kidogo ananigeuka na kusambaza sifa chafu kuhusu mimi. Nimeamua kuingia studio mwenyewe na nimekamilisha singo yangu inaitwa '2009' pale Sound Crafters. Nawazungumzia wasanii wenye tabia za unyenyekevu na baadaye dharau. Mwezi ujao itakuwa mtaani."

Alipoulizwa kama ameanza kutuma ujumbe mfupi wa vitisho kwa wasanii hao, ?Wanaweza kusema hivyo, nimetuma ujumbe kuwakumbusha mengi niliyowasaidia na jinsi nilivyowainua. Sitaki tena mambo ya namna hii, yalianza kutokea wakati wa (Juma), Nature. Leo hawa, sina hata amani nahisi tena kuna wengine pia wanakuja na watafanya hivyo,? anasema Fela maarufu kama ?Mkubwa?.

















Na Mussa Mkama

UNAPOZUNGUMZIA wachezaji makinda katika timu ya soka ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', huwezi kulikosa jina la kiungo wa Yanga, Kigi Makasi.

Licha ya kuwa si mchoyo wa pasi, Kigi ni mchezaji mwenye kipaji cha pekee, ila utampenda zaidi kutokana na mbio zake uwanjani, ujanja wa chenga na mashuti.

Huwezi kuamini ukiambiwa mchezaji huyo mwenye umbo dogo aliyekuwa akichezea Mtibwa Sugar kabla ya kutua Yanga kuwa ana umri wa miaka 18, na hilo linadhihirisha kuwa umri si jambo la muhimu zaidi ya kipaji uwanjani.

Sifa nyingine ya kuwa mpole, kuelewa mafunzo ya kocha, kasi yake uwanjani, uwezo wa kumiliki mpira na uwezo wa kukaba ilimfanya ajikute akiitwa na kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo katika kikosi hicho.

Kama Maximo mwenyewe ambavyo amekuwa akisema mara kwa mara kuwa mmoja ya sifa ya kumuita mchezaji katika kikosi chake ni nidhamu, hakuna shaka kuwa Kigi anafuzu kwa hilo na hasa ukizingatia kuwa anajituma wakati wote uwanjani.

Mara kadhaa amekuwa akiingia dakika za mwisho wakati Stars inacheza, lakini ndiye amekuwa akifunga magoli muhimu licha ya kucheza dakika ishirini za mwisho za mchezo. Kigi anasema malengo yake ni kucheza soka la kulipwa Ulaya na ikiwezekana awe mchezaji bora wa Ulaya jambo ambalo ameahidi kuwa linawezekana kwani awali aliiahidi kuicheza Taifa Stars na ametimiza.

Anasema umri wake bado unamruhusu kufanya makeke ya kucheza Ulaya na kwamba atazitumia fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani kuonyesha kipaji chake ili anunuliwe na mmoja ya klabu za Ulaya. Nje ya uwanja, Kigi anasema hana mpango wa kuoa mpaka lengo lake la kucheza Ulaya likamilike.

Hata hivyo amesema njia ya kwenda Ulaya sasa ni wazi kwani kufuzu kwa Stars katika fainali hizo kumefungua milango kwa mataifa makubwa yaliyoendelea kisoka kutuma wakala wao Ivory Coast kusaka wachezaji. Kigi aliyezaliwa mwaka 1990 katika kijiji cha Nalipungu mkoani Mwanza, alisoma Shule ya Msingi Nalipungu katika mkoa huo.

Mchezaji huyo alijiunga na Shule ya Sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam ambako alionyesha kipaji chake kilichowavutia Mtibwa Sugar aliyojiunga nayo. Kigi aliyejiunga Yanga msimu uliopita anaishi Kimara jijini Dar es Salaam ambako anadai ni rahisi kwake kujiendeleza kuliko angekuwa mkoani.

?Unajua Dar es Salaam ndio kila kitu, kipaji changu kwa mara ya kwanza kilitambulika hapa na ndipo niliposajiliwa na Mtibwa Sugar, hivyo jiji hili nalihesimu kwani ndilo lililonipa maisha na ninaamini kupitia hapa nitafika safari yangu." Mwisho ......e&p....2008/12/29
Ndani ya Mwanachi News,