Friday, April 24, 2009


RUKA KWELI PAMBA WASILIANASI +255717749581

New Tops nazo bei moja na tshirt Ruka in tanazania vaa pamba za kijanja kwa sh/=15000 karibuni wote..
New tshirt Ruka in tanazania vaa pamba za kijanja kwa sh/=15000 karibuni wote..
New tshirt Ruka in tanazania vaa pamba za kijanja kwa sh/=15000 karibuni wote..





New tshirt Ruka in tanazania vaa pamba za kijanja kwa sh/=15000 karibuni wote..
Nakaaya awalaumu Fid Q Klynn
Nakaaya awalaumu Fid Q na Klynn
Inasemekana kwamba mwanadada Nakaaya amekerwa sana na kitendo cha wasanii wawili kutomuonesha ushirikiano katika kazi. Habari zinasemea kuwa Nakaaya aliwaomba wasanii wengi wakali wajitokeze studio wakati wa kurecord wimbo wake wa 'I am an African' na kuingiza sauti zao katika ngoma hiyo, lakini Fid Q na K-Lyinn walishindwa kutokea

Wimbo umekamilika bila ya sauti zao na video pia ipo tayari, waliyoshirikishwa katika ngoma hiyo ni Chidi Beenz, Lufunyo na wengine.


Kwa upande mwingine Fid Q aliteta na DJ Fetty wa Clouds FM na kumuambia "Nakaaya alinipigia simu mida ya mchana na kuniambia niende studio saa hiyo, ndio nikamwambia angeniambia mapema maana nilikua mjini na mihangaiko mingine na nisingeweza kufika studio saa hiyo hiyo aliyonipigia simu. Unajua Fetty mi hayo mambo nilishaacha zamani nikajirekebisha nisengependa kurudi huko. Hata kama ni wewe Fetty mtu anakupigia simu saa hiyo hiyo anataka uende studio hautaweza kweli kwasababu tayari unakuwa na mipango yako kichwani. Angeniambia kabla ningeenda, kwanini nikatae?!".

Kama hayo ni kweli, hatuoni sababu ya kujenga chuki kwa vile ni mambo ambayo yanatokea...wasanii wetu waendelee kufanya kazi kwa moyo mmoja.
Uwanja wa Taifa huenda ukafungwa



Uwanja wa Taifa huenda ikafungwa
Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imesema huenda ikalazimika kusimamisha matumizi ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hadi pale atakapopatika mzabuni wa kuuendesha

Akizungumza katika mahojiano maalum na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Florens Turuka alisema kuwa uamuzi huo unaweza kufikiwa kutokana na serikali kutumia gharama kubwa za uendeshaji wake tofauti na mapato yanayoingia.

"Tunaweza kusimamisha kabisa matumizi ya Uwanja wa Taifa mpaka hapo mzabuni atakapopatikana, hii inatokana na serikali kutumia fedha nyingi za uendeshaji wake huku mapato yanayopatikana hayatoshelezi,"alisema.

Alisema kuwa wizara yake inashangazwa na mapato kidogo yanapopatikana uwanjani hapo licha ya mashabiki wengi kuonekana kuhudhuria mechi hali inayowapa wasiwasi kuwa huenda kuna namna fulani ya hujuma inayofanyika kwa manufaa ya watu wachache.

"Unajua kuona ripoti ya mahudhurio ya watu ikiwa juu halafu mapato yanayopatikana ni madogo, hilo linatupa wasiwasi labda kuna hujuma fulani inayofanyika na ndio maana tunataka apatikane mzabuni tutakayemkabidhi mamlaka ya kusimamia ili uwanja uwe ni kwa faida ya umma na si watu wachache,"alisema Dk Turuka.

Dk Turuka alisema kuwa kinachosubiriwa kwa sasa ni kumalizika kwa muda wa zabuni iliyotangazwa ili waweze kupitia majina ya waombaji na kuangalia sifa zinazotakiwa kabla ya kumtangaza aliyeshinda.

Katika hatua nyingine, DkTuruka alisema kuwa leo anatarajia kuutembelea uwanja huo ili kuangalia kama kuna kasoro yoyote ili ziweze kurekebishwa.