Friday, July 31, 2009


Lady Jaydee a.k.a Manka

ambaye anamiliki bendi iliyoko juu kwasasa Bongo “Machozi Band” inyotumia mtindo wa “Sanya Sanya” amesema anategemea kusimamisha maonyesho yake kwa kipindi cha mwezi mmoja kupisha mfungo wa mwezi wa Ramadhani ambao unakaribia.

Katika waraka wake nipehahabari iliyoupata Jaydee amesema wameamua kusimamisha maonyesho hayo kwa kipindi hicho kutokana na kuwaheshimu na kuwasindikiza waislam wote kwenye mwezi huo.

Akiongeza Jaydee alisema pia atatumia fursa hiyo kwenda likizo baada ya sanya sanya ya muda mrefu toka mwaka uanze bila kupumzika.

“Japokuwa wanasema mlalahoi hana sikukuu, nahitaji hata mwezi mmoja nikatulize akili mahala mbali na nyumbani, ila kwakuwa kwetu mteja ni mfalme nawasikiliza nyinyi maoni yenu na kama mtatasisitiza nipige kazi basi sina budi zaidi ya kutimiza mtakachosema” alisema Jaydee

Jaydee pia aliwaambia watu sababu gani siku hizi anaitwa Manka.

“Unajuwa tulijipa haya majina mimi na wadogo zangu watatu ambao ni Kimario (Mwana FA) Massawe (AY) na yeye mwenye Manka(Jaydee), hii tuliitumia kama inavyojulikana ndugu zetu wachaga walivyo hodari katika kutafuta basi na sisi tunafwata nyao zao” alisema Jide

No comments:

Post a Comment