Nani Mkali wa Freestyle Bongo..??
Mratibu wa shindano hilo DJ Fetty alisema ya kuwa wanategemea mashindano hayo kufanyika mwishoni mwa wiki hii ndani ya ufukwe maarufu kabisa wa Coco Beach ambapo shindano liko wazi kwa yeyote yule anayetaka kujitokeza kushiriki kwa Wilaya ya Kinondoni kwanza na baadae itafuatia kwa wilaya za Ilala na Temeke.
“Kama nilivyosema tunategemea shindano litafanyika Coco Beach kuanzia muda wa saa tatu asubuhi siku ya tarehe 8 ambapo mshindi atakaepatikana hapo ataingia kwenye Fainali ya mikoa yote mitatu, form zipo ofisi zetu za Clouds FM Mikocheni au Kitega Uchumi” alisema Fetty
Bila kuweka ni kiasi gani mshindi wa kwanza atapata lakini Fetty alisema ya kuwa kuna mamilioni ya zawadi na hivyo basi kama unajiamini wewe ni mmojawapo fika Coco uchukuwe Mamilioni hayo.
No comments:
Post a Comment