Sunday, September 6, 2009


VIJANA NAO WANENA KUHUSU UCHAGUZU MKUU

Walia na vijana kutopiga kura .takwimu zaonesha hawapigi kura bila sababu - Asasi isiyokuwa ya Kiserikali inayotambulika kama Dira ya Vijana (TYVA) imetoa tamko linalowataka vijana wote kutilia maanani na kuthamini ulazima wa kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.

“Vijana wengi wana kadi lakini hawapigi kura. Kwa mfano nilimuuliza kijana mmoja akaniambia hawezi kuwapigia mafisadi kura, huu ni mtazamo finyu, sisi ndio tunaotakiwa kulikomboa Taifa na suluhisho ni kushiriki kuchagua viongozi waadilifu� alisisitiza Ngoja Mjumbe wa kamati ya Asasi hiyo.

Siku chache zilizopita Asasi hiyo yenye matawi mikoa mbalimbali nchini, iliitisha mkutano uliowakutanisha vijana kutoka sehemu mbalimbali tarehe 22 mwezi uliopita katika ukumbi wa Peacock Millennium Tower kujadili kwa kina pia kutoa mapendekezo mbalimbali kuhusu uchaguzi huo.

Pamoja na mambo mengine, walihimiza vijana kushiriki bila kukosa kuwachagua viongozi bora, kamati kuu ya uchaguzi (NEC) kutoa taarifa sahihi kwavijana na umma kuhusu uchaguzi huo, huku wakivitaka vyama vya siasa kuwapitisha vijana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

No comments:

Post a Comment