Wednesday, July 21, 2010

Daladala yauwa wanafunzi wawili leo asubuhi
wanafunzi wawili mtu na ndugu yake ambao majina yao hayakuweza kujulikana  wamegongwa na daladala maeneo ya njia panda ya kuelekea bahari beach na daladala ya kunduchi na kufa papo hapo.
Baada ya tukio hilo wnafunzi wenzake(shule hatujapata jina)walikuja juu na kufunga barabara  ya kuelekea tegeta ambayo ilisababisha foleni mana hakuna gari lililopita kwa takribani saa 1 na 30 hivi.
 
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa asubuhi hii.
Angalia video hapo chini ujionee mwenyewe
Habari katika video hapo juu imekuwa fupi kwa sababu mdau aliyetuletea ilibidi aondoke mapema eneo la tukio mana wanafunzi walikuwa wanarusha mawe sana.
Picha na habari tumetumiwa na mdau wetu wa blog Baba styles

1 comment:

  1. TZ TZ TZ inaelekea wapi? mbona mambo mkorogano maajali yasiyoisha mara majambazi mara mara alibno mara rushwa mafisadi mara hali ngumu ya maisha sasa mtanzania ataponea wapi?nchi imekuwa mkorogano inabidi watanzania tusali sana nchi imeoza imenuka sisi tuliye bahatika kuwa nje ya nchi hatuna hamu ya kurudi huko japo nyumbani ni nyumbani km alivyoimba remmy ongala lakini nikiangalia haya matukio ndiyo nazidi kukata taama kbs japo natamani sana nyumbani

    ReplyDelete