Ukipitapita mchana ndani ya Jiji la Dar-es-Salaam, utakuta Vijana wengi wamelala kando ya barabara chini ya miti, wameuchapa usingizi mzito mithili ya mtu aliyekufa. Ukiwauliza; eti wanapunga hewa; Kazi wanafanya muda gani? Eti hakuna ajira! Je, wanaishije kama hawana ajira? Hakuna jibu la msingi watakalokupa.
Ama hawa ndo VIBAKA? Wanalala mchana na kukaba usiku? Kijana Jamadari mwenye nguvu na uwezo wa kufanya kazi huwezi kusema hakuna ajira. Na wengi wao wametoroka vijijini kulima na kufuga, huu ni UVIVU na kupenda njia za mkazo (short cut life). Manispaa ya Jiji inabidi iliangalie hili, na si kukimbizana na MAMA NTILIE na MACHINGA wanaojitafutia ridhiki zao kwa uwezo wao.
No comments:
Post a Comment