Wednesday, July 28, 2010

WATU 12 WAHOFIA KUFA CHINA
Watu 12 au zaidi wanahofia kufa na mamia kujeruiwa baada ya mlipuko uliotokea katika kiwanda cha plastiki mashariki mwa chini.kipande cha video kilichokuwa kinaonyeshwa katika televisheni ya taifa nchini china ilionyesha moshi mzito uliokuwa umetanda katika mji wa Nanjing baada ya mlipuko Karibu na kiwanda hicho.
Hospitali nyingi ziliishiwa na damu ikabidi kuomba watu zaidi kuchangia kutokana majerui wengi zaidi kuhutaji damu ya ziada.Watu zaidi ya 300 walihitaji ungalizi wa karibu zaidi,ikiwemo watu 52 waliumia vibaya sana,vyombo vya habari nchini china viliripoti.

No comments:

Post a Comment