AJARI TENA
Ajari ya pikipiki maarufu kama boda boda imetokea leo asubuhi maeneo ya mbezi karibu na darajani kama inavyoonekana kwenye picha hapo juu.Pikipiki ilikuwa na dereva na abiria mmoja,mdau aliyetutumia hii picha alikuwa kwenye daladala ameiambia blog yenu kuwa mtu mmoja amepasuka vibaya maeneo ya nyuma ya kichwa na hakuweza kujua kuwa alikuwa ni dereva au abiria.
Ajari za pikipiki siku hizi zimeongezeka sana maeneo haya ya mbezi mpaka kunduchi na sababu kubwa ni uendeshaji kasi usiofuata sheria za barabarani wa madereva wa pikipiki.
No comments:
Post a Comment