Mr ibrahim bicacki akiongea wakati wa uzinduzi wa feza alumni
Jumapili ya tarehe 29 mwezi huu Jumuiya ya Feza alumni ilizinduliwa rasmi katika ukumbi wa Istana Victoria.Uzinduzi huu uliwashirikisha wanafunzi wote waliowahi kusoma katika shule ya Feza toka mwaka 1998. Hii inaonyesha wazi jinsi gani shule ya Feza imelea na inaendelea kulea vijana wa kitanzania wanaopitia mikononi mwao kwa upendo na maadili mema, ili wawe raia ama viongozi bora nchini.Pia kuwafundisha kuwa wana wajibu na haki ya kusaidia jamii yetu ili kuishi kwa amani,upendo na kuleta maendeleo ya kweli.
Jumuiya hiyo ya Feza Alumni inaundwa na vijana hao wa kitanzania, waliomaliza katika shule ya Feza, ikiwa na lengo la kutoa huduma kwa jamii. Jumuiya itajihusisha na harakati za kuleta maendeleo katika sekta ya elimu, utamaduni na afya. Akizungumza na waandishi wetu wa habari, bwana Ibrahim Yunus Rashid ambaye ni Mwenyekiti na mwanzilishi wa jumuiya hiyo alisema,
Mr.Ibrahim yunus wa pili kutoka kulia akiwa karibu na mgeni rasmi
“Mimi ni katika wanafunzi wa mwanzo tangu shule ilipofunguliwa mwaka 1998. Na nilimaliza mwaka 2001. Na sasa hivi nikiwa ni mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, nimeona umuhimu wa kuwahimiza wenzangu tukusanye nguvu zetu kwa ajili ya jamii. Elimu tuliyoipata inabidi tuirudishe kwa jamii, na si kwa njia nyingine yeyote isipokuwa kwa kuitumikia jamii.”
Wakiwa na mipango kadhaa kwa ajili ya jamii, jumuiya ya Feza Alumni tayari wameshaanza harakati zao pale ambapo tarehe 28 mwezi huu waligawa misaada ya chakula kwa vijiji saba vya wilaya ya bagamoyo katika mkoa wa pwani. Na tayari wameweza kuwakaribisha jumuiya za kigeni kutokea marekani kwa ajili ya kuja kugawa vyandarua, zoezi ambalo litafanyika hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment