Saturday, October 30, 2010

KWA WAKAZ WA DAR
we thank you all of our customers from various places in Tanzania and those who have been in and outside country for your generous hearts,,maximum apreciation which gives us strength to carry on..bado tutafanya sana...tell your friend, book your apointment mapema..and we work..nashkuru sana..


you can start calling our regular numbers for apointments
+255 717 362 724
+255 753 838 258
+255 788 352 162.
ukitaka kujua kazi zao zaidi kujiridhisha kwamba hawa jamaa ni wakali ingia
http://www.bodyartarusha.blogspot.com/
KARIBU..
Happens today
Experts say efforts to beat malaria may backfire
The mosquito is responsible for carrying the malaria parasite from human to human
Efforts to eradicate malaria in some countries may be counter-productive, an international team of researchers suggest.

In the Lancet, they suggest some countries, particularly in sub-Saharan Africa, may be better pursuing a policy of controlling the disease.
They also criticise the World Health Organization (WHO) for not providing adequate direction.
But a WHO spokesman said beating malaria must remain the ultimate goal.
South African inmates ask for circumcision to fight HIV
The authorities in South Africa's KwaZulu-Natal province say they have been "overwhelmed" by the number of prisoners wanting to be circumcised to help combat the spread of HIV.

Some studies suggest being circumcised can help men halve their chances of contracting the Aids virus.
KwaZulu-Natal has one of the highest HIV infection rates in South Africa.
Provincial health minister, Sibongiseni Dhlomo, said only volunteers were being circumcised.

"We've had more people wanting to be circumcised than our resources can actually manage. In fact, we're overwhelmed," Mr Dhlomo told the BBC.
He said the targeting of prisoners was part of a wider programme to circumcise sexually-active men in the province, and that the idea to extend it to prisons had come from the inmates themselves.
For more story follow the link
Man Utd suffer Wayne Rooney blow, Alex Ferguson admits
Rooney was injured in training before Man Utd's game with Bursaspor
Manchester United manager Sir Alex Ferguson has admitted that Wayne Rooney could be out for longer than the three weeks initially expected.

The 25-year-old striker is currently on holiday as he recovers from the ankle injury he picked up in training.
Rooney recently signed a new five-year deal to stay at Old Trafford days after he said he wanted to leave the club.
Asked if three weeks was still the prognosis for his return, Ferguson said: "I think it may be longer."
Ferguson added: "There is no recovery, it is just rest.
DR.Kikwete aongea na wananci kupitia wanahabari jana usiku 
JK akiongea na waandishi na wageni waalikwa katika mkutano wake na waandishi wa habari.

baadhi ya waliohudhuria mkutano huo katika ukumbi mkongwe wa Arnautoglou


Friday, October 29, 2010

Tupime-tujue club
THOMSON.M.SANGA,(Muasisi na mlezi tupime-tujue club)
Thomson sanga “vijana tunachangamoto nyingi sana katika uliwengu wa sasa na inatubidi tuwe waangalifu ili kuweza kukabili-ana nazo.Kuna magonjwa mengi na vishawishi vingi ambavyo vinachochea katika kuturudisha nyu-ma kielimu na kimaisha.
Wakati wa kumtegemea mtu mwingine asimame badala yetu umekwisha na hatunabudi kuungana kwa pamoja ili kuzikabili changamoto hizi.

Shule ya sekondari lugoba imenipa mwangaza katika kuweza ku-shirikiana na vijana wenzangu ili kutafuta mbinu mbali tunazoweza kuzitumia katika kukabiliana na changamoto zinazotukabili sisi vijana kwa ujumla.
Naomba wewe kijana na jamii kwa ujumla tutambue kuwa UKIMWI ni changamoto namba moja ambayo tun-atakiwa kuikabili bila kukata tama a na kurudi nyuma.

Mimba za utotoni ni jambo ambalo hatuna budi kulipiga vita kwani huyu kijana anayeharibiwa maisha yake leo ni hasara kwa taifa la leo na kesho pia”
Binafsi naamini “vijana bila ukimwi inawezekana”na “vijana tunaweza endapo tutapewa nafasi”.

MAHALI TULIPO.

Tupime-tujue club tupo kilomita 23 pembezoni mwa barabara iendayo tanga kutoka chalinze.Tupo shule ya sekondari lugoba
          
“Vijana tuna nafasi kubwa ya kuhakikisha tunaweza kujilinda na kuepuka vishawishi na vikwazo vinavyoweza kutukwamisha katika kutimiza ndoto zetu za kuwa wanasheria, walimu,mainjinia,madaktari n.k.

Wengi wetu tumezoea mfumo wa kusubiri kusemewa na watu wengine kama wazee,wazazi na walimu.Wakati umefika sasa kwa sisi kuweza kujitambua na kujilinda na vikwazo na mazingira ya ulimwengu huu wa sasa wa sayansi na teknolojia.Kwa kushirikiana tunaweza na kwa msaada wa jamii zetu tunaweza kufanikiwa zaidi.
Tusisubiri kila kitu kusemewa na watu wengine kwani uwezo tunao,nia tunayo na sababu pia tunazo.Tuamke sasa!!!”
“Vijana wa wakati huu ni tofauti na vijana wa zamani,sayansi na teknolojia ya karne hii pamoja na utandawazi vinachangia kutufanya tubadilike.Pamoja na haya yote ni jukumu letu wenyewe kujilinda na kujiweka katika hali ya usalama ili kulinda mila na desturi za nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa magonjwa sio sababu ya kufanya ndoto zetu zisitimie”

MELKIORY JOHNBOSCO;
(Mwenyekiti 2008-9)
Jay-Z Responds to Beyonce Pregnancy Rumors “It’s not going to happen,”
Jay-Z Responds to Beyonce Pregnancy Rumors “It’s not going to happen,” Jay-Z told Australia's Daily Telegraph. “I’m just shooting down the rumors before they start.”
“They do that every slow news day," Hov continued. "This is like the fifth time. I think we have five kids now. No truth, but I wonder when people will stop giving it relevance? You can’t do the same subject. At least change the subject, they have to find a new one.”


While rumors of a pregnant Beyonce have been circling around for years, things reached bigger proportions last week with outlets confirming the news rather than speculating. Bey's mother, Tina Knowles,I’m here to clear the rumors up. The truth is that it’s not Beyonce that’s pregnant, it’s me,” Mama Knowles told Elle DeGeneres before quickly adding, “I’m kidding, I’m 56.”
The largest city Tanzania

Formerly Mzizima,is the largest city in Tanzania.It is also the country's richest city and a regionally important economic centre.Dar es Salaam is actually an administrative province within Tanzania,and consists of three local government areas.










Ukitaka kuijua Dar es slaam zaidi kupitia facebook fuata link
NEW UPCOMING ALBUM from
YOUNG DEE

ITS YOUNG DEE WITH HIS NEW UPCOMING ALBUM KNOWN AS YOUNG RAPPER FROM NEW FISHCRAB COOKOUT(AUDIO STATION).............HE NID YOUR SUPPORT- PHOTOGRAPHY BY RAQEY FROM EYEVIEW
 N ARTWORK BY ME TAZ TOZ
Sembuse wewe? 31th oct Tukapige kura
Kama wazee hawa walithubutu kusimama kwenye msururu mrefu hivi ili wapige kura, itakushinda nini wewe baba,wewe mama,wewe kaka,wewe dada wewe kijana,kusimama foleni na kupiga kura shimeshimee watanzania tukapige kura,mabadiliko yataletwa na kura yako.katika picha hapo juu wa nne kushoto ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akiwa kwenye foleni ya kupiga kura
Jaydee has been nominated to Uganda's PAM awards
Jaydee has been nominated to Uganda's PAM
awards - Best Female Artist from Tanzania category http://www.ugandaonline.net/pamawards/?y=2010&m=10

Gardner G Habash "Wadau na Friends, Jide amechaguliwa tena PAM Awards - Uganda, katika kundi la msanii bora wa kike. PLS naombeni kura zenu kijana aulete mzigo home. Jinsi ya ku vote unaandika 36 unaacha nafasi unaandika LADY JAYDEE unatuma kwenda namba +256 752 600 100. "

Thursday, October 28, 2010

STREIKA FOR SALE
A tour to fight Malaria in Africa

Urban Pulse Presents The urban tour which is aimed to promote & fundraising Money to fight Malaria in Africa. The Tour will Feature The best Bongo Flava Artist who is the ambassador for Malaria in Tanzania Diamond alongside Mish the fyah sis From Urban Pulse Creative 6th Nov Milton Keynes, 12th Nov @the club London 27th Nov In Birmingham
If you would like to help please write us on
urbanpulseCreative@googlemail.com.
Owen - I could call it a day
Michael Owen admits he could hang up his boots if Manchester United release him at the end of the season.


The former England international is in the final term of a two-year deal at Old Trafford and has not yet entered talks with manager Sir Alex Ferguson over a possible contract extension.
Owen has been struggling with injuries of late, with a fresh hamstring tweak keeping him on the sidelines for a further month after a groin problem hindered the start of his campaign
Angalia hii clip (Nataka ucheke)
Watanzania wakati umefika wa kutumia faceBook ipasavyo

Watanzania wakati umefika wa kutumia faceBook ipasavyo kwa kuleta Maendeleo Nchini Mwetu. Tukiwa kama Jumuiya ya Watanzania tuishio ughaibuni Tumeamua kutengeneza Special Page kwa ajili ya kujadili mambo muhimu ambayo yanaweza kuleta maendeleo nchini mwetu. hasa , kwa kukosoa na kutoa solutions nini tunapaswa kufanya katika idara zote, ilituwe kama wenzetu USA, CANADA, CHINA , JAPAN , SOUTH AFRIKA ,UK ETC.

Kutokana na uchunguzi tulioufanya % ( asilimia ) Kubwa ya watanzania wamejiunga na mtandao wa Face book. Na tunatumia mda mwingi sana katika hii page kwa siku. Tukiwa kama watanzania tulio na uchungu wa maendeleo tumetengeneza special page iitwayo
DAR ES SALAAM, TANZANIA.

http://www.facebook.com/profile.php?id=100000492651030&ref=pymk#!/pages/Dar-es-salaam-Tanzania/147302971966158

Unachopaswa kufanya ni kujiunga na hii page ( kwa kupofya LIKE)
Kisha utakuwa ushajiunga directly , na utaweza kutoa ushauri wako wa busara katika wall paper ya hii page. Ukiwa na picha ya maeneo yaliopo Nchini mwetu ambayo yanahitaji msaada wa ziada itakuwa ni vizuri zaidi kwani watu ( watanzania wote waliojiunga tunaweza toa ushauri kutokana na swala husika).

Unaweza suggest hii page kwa marafiki zako. wenye busara na hekima.
Ni jukumu letu sote kuleta mabaliko na maendeleo Nchini mwetu. Kuna watu wanadata za kutosha ila wanashindwa njia rahisi yawakuwafikishia walengwa wakati umefika sasa.
Naamini tukiitumia hii page ipaswavyo tunaweza leta maendeleo nchini kwa njia moja au Nyingine.

Busara na hekima yako itachangia kwa asilimia kubwa wakati umefika wa mabadiliko.
Mabadiliko tutaleta sisi Wenyewe. inahitaji uzalendo na kujitolea kwa ajili ya nchi yako
Wenu:
Wadau Ughaibuni
A tribute to Lucky dube this 29th Oct 
 KESHO

I-Noch brings you the Live performance “Explosive Zion “ a Reggae Live concert with Zanz-B from Jamaica supported by local Ragga , Raggae and Dance Hall artists .
Performances from Jhikoman and Afrikabisa Band, Saganda and Hardmad accompanied with “Zemkala Band”

Venue: Makumbusho Cultural Center
Date: 29th October 2010
Time : 7pm till dawn.
"Tickets Available at the Gate."

Wednesday, October 27, 2010

Behind the scenes of "take the people away" video
Leo nazizi amefanya video ya wimbo wake "take the people away".Na hivi ndio ilivyokuwa wakati wa shooting.Hapa nazizi akiwa anapata make ups kabla ya ku shoot.



Make up imeshalala kwenye sura sura ya nazizi,kinachofuata ni mzigo mzuri kutengeneza.






Wenger taking no chances
Arsene Wenger has urged Arsenal to 'go for everything' this season as they look to end their silverware drought.


Wednesday evening will see Wenger's men travel to Newcastle in the Carling Cup, a tournament which, along with the FA Cup, has taken a backseat to the Premier League and UEFA Champions League at Arsenal in previous campaigns.

However, with the Gunners having failed to lift to a trophy for five years, manager Wenger accepts his side must make the most of every opportunity to secure another title.
Man Utd hero Javier Hernandez earns Ferguson praise
Sir Alex Ferguson heaped further praise on Javier Hernandez after his 90th minute winner propelled Manchester United into the quarter-finals of the Carling Cup on Tuesday night.



The Mexico international was the United hero for the second time in as many days after he came off the bench to sink Wolves at Old
Trafford.Hernandez, who scored twice at Stoke on Sunday, stepped off the bench to give United a 3-2 victory at home to Wolves.
Mkutano wa Kampeni Kiwalani Jimbo la Ukonga (Segerea): Mahanga ajivunia shule za sekondari za kata

Mgombea ubunge wa Jimbo la Ukonga (sasa Segerea) Mheshimiwa Makongoro Mahanga amejivunia mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye miaka mitano iliyopita ya upanuzi mkubwa wa elimu jimboni hapo.


Alisema ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010 imefanikisha ujenzi wa shule za sekondari 34 na kufanya jimbo hili kuongoza nchi nzima kwa ujenzi wa shule nyingi mpya nchi nzima.
Aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambapo leo yuko kwenye Mkoa wa Dar es salaam kwa ajili ya kunadi sera za CCM na kuomba wananchi ridhaa ya uongozi.


Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, kabla ya kumkaribisha Mheshimiwa Kikwete kutoa hotuba yake ya kampeni, alichukua nafasi hiyo kuwasihi wananchi wa Kiwalani kuchagua CCM na wagombea wake. Pia alimuahidi Mheshimiwa Kikwete kwamba CCM mkoa watajitahidi ili CCM ishinde kwa kishindo, majimbo yote nane ya Mkoa wa Dar es salaam.


Kwenye hotuba yake ya kampeni Mheshimiwa Kikwete alisema CCM ni waaminifu na wakiahidi wanatekeleza ahadi zao hivyo wachague CCM iendelee kuongoza.


Aliongeza kuwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2005 - 2010, elimu ilipewa kipaumbele na kupewa asilimia ishirini ya bajeti ya serikali. Lengo la serikali ya CCM kutenga bajeti hiyo kubwa ni kukabiliana na changamoto zilizopo ili bajeti hiyo ikidhi mahitaji yaliyopo.


Akielezea mpango wa uboreshaji wa huduma ya afya, Mheshimiwa Kikwete alieleza kuwa mwaka 2005 CCM iliahidi Watanzania, itasogeza huduma za afya karibu na wananchi walipo na lengo ni kuwa Mtanzania asisafiri zaidi ya kilometa tano kufuata huduma ya afya.


"Ndipo CCM ilipoanzisha mpango wa kujenga zahanati kwenye kila kata, na kwa kipindi cha miaka mitano inayokuja 2010 - 2015, zahati hizo zitapandishwa hadhi kuwa vituo vya afya, na kwa miji kama Dar es salaam, vituo hivyo vitakuwa hospitali ndogondogo". Alisema Mheshimiwa Kikwete.


Mheshimiwa Kikwete pia alizungumzia mpango wa upatikanaji wa huduma ya maji ambapo alisema jiji la Dar es salaam lina upungufu mkubwa wa maji kutokana na ongezeko la watu mijini.


Kwa upande wa miundombinu ya barabara, Mheshimiwa Kikwete alisema jitihada mbalimbali zimefanyika ili kukabiliana na changamoto iliyopo mijini kuwa na magari mengi kwa kufanya upanuzi wa barabara kubwa. "Lakini mpango mkubwa uliopo sasa ni wa kujenga barabara za juu "fly-overs" ambazo zitasaidia sana kupanga mji na pia kupunguza tatizo hili sugu.


Mheshimiwa Kikwete pia alielezea jitihada mbalimbali za serikali yake kuwainua wananchi kiuchumi ikiwemo mifuko ya fedha na uwezeshaji wa vijana kupata ajira.
Mwishoni Mheshimiwa Kikwete alimnadi Dkt Makongoro Mahanga ambaye ni mgombea ubunge wa jimbo la Segerea na madiwani wa kata zote jimboni hapo.
Mkutano wa Kampeni Nyamagana:
Umati mkubwa wafurika kumsikiliza JK
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wananchi wa jimbo la Nyamagana alipowasili kwenye mkutano wa kampeni jana jioni .

Umati uliofika kumsikiliza dr.kikwete jana jioni


Mapokezi makubwa yamemkaribisha Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mgombea urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza jana jioni.


Kwenye mkutano wake wa kampeni Mheshimiwa Kikwete alisema CCM ni chama kinachohubiri amani, utulivu na mshikamano na sio chuki na kupigana vita. Hivyo Watanzania wawape nafasi ya kuendelea kuongoza nchi kwa awamu nyingine tena. Alibeza vyama vya siasa vilivyoshindwa kuelezea sera zao na kuhubiri chuki au kutangaza vita.


"Siasa ni ushindani wa sera na mipango ya maendeleo na sio kushindana kurusha mawe na kutupiana matusi kwenye majukwaa" Alisema Mheshimiwa Kikwete huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wana Nyamagana waliofurika kwenye uwanja wa Sahara Kata ya Pamba, jimbo la Nyamagana.


Mheshimiwa Kikwete aliyetokea Chato mkoani Kagera, alielezea jitihada za CCM za kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania kwa kuboresha huduma za jamii. Alielezea mpango mkubwa wa kusaidia vijiji kumi na mbili vya wilaya hii ya Nyamagana kupata maji safi na salama, unaofadhiliwa na benki ya dunia.
"Miji na Vijiji kumi na nane vitapatiwa umeme katika mkoa huu wa Mwanza ikiwemo Nyamagana na Ukerewe" alieleza Mheshimiwa Kikwete wakati akielezea mpango mkubwa wa kuboresha huduma ya umeme.


Huduma nyingine alizozitolea ufafanuzi ni ile ya ujenzi wa barabara, kilimo kwanza ili kuendeleza wakulima na wafugaji, upanuzi mkubwa wa elimu n.k.


Kabla ya kuhutubia mkutano huo mkubwa wa kampeni, mgombea ubunge wa Jimbo la Nyamagana Mheshimiwa Lawrence Kego Masha aliwahimiza wananchi hao kuwa makini na vyama ambavyo havitawaletea maendeleo na kuwasihi wachague CCM.