Mie nadhani tatizo ni uchanga wa wasanii wanaotoka hivi karibuni kutokuwa na uelewa wa tasnia ya muziki na jinsi ya kujiendesha ndio kunawafanya kutafuta meneja yyt Yule ili mradi apate mtu wa kumsimamia kazi zake.Ukiangalia kwa undani zaidi wengi wa mameneja wanafanyia uzoefu tu,yani kwa sababu yeye ni producer,dj,presenter au amekuwa karibu na watu wanaohusika na muziki basi ndio kigezo cha kummiliki msanii.Mie nadhani wakati wa mambo kama haya umeshapita na sasa ni muda wa kutafuta watu waliosoma na kuelewa kuwa biashara na muziki vinaenda sambamba,pia kupata watu ambao wataweza kusoma alama za nyakati na kuwaelekeza wasanii nini cha kufanya kutokana na muda!
Ilikujua zaidi mambo yanayotokea kati ya wasanii wakongwe na chipukizi,nilipata kukutana na baadhi ya wasanii wakongwe na chipukizi na kuwauliza maswali.Walikuwa wako tayari kunijibu kwa kigezo cha kutotajwa majina yao kabisa.Nitatumia mkongwe(Nikimaanisha msanii mkongwe) na Chipukizi(Msanii chipukizi)
Nipehabari: Hivi ni kwanini nyie wasanii wakongwe hamuwashirikishi baadhi wasanii wachanga katika nyimbo zenu ,mana siku hizi wao ndio wapo juu zaidi?
Mkongwe: Sio kwamba hatutaki kuwashirikisha ila wanaojiita mameneja ndio wanasababisha haya yote yatokee mana huwazuia kufanyakazi na msanii yeyote mpaka wapate ruhusa kutoka kwao.Kwa mfano hivi karibuni nilitaka kufanya kazi na msanii X (jina nimelihifadhi) ,nikatafuta namba yake ya simu na kumpigia alichonijibu ni yeye hawezi kufanyakazi na msanii yeyote mpaka niongee na meneja wake.
Ikabidi nimpigie simu meneja wake alichonijibu ni kwamba msanii X hafanyikazi na msanii yeyote mana kuna project anafanya kwa sasa,ataangalia labda akishamaliza hiyo project. Nilishangaa sana na nilikuwa na maswali mengi ya kujiuliza ambayo nilikosa majibu.
Kitu ambacho wasanii wachanga na mameneja hawajui ni kwamba kwa wasanii wakubwa kuwashirikisha katika nyimbo zao kwanza kunawaongezea umaarufu na uzoefu na pia wasanii wachanga wanapata nafasi ya kuwapata mashabiki wangu na kuwa wakwake pia.Nadhani inabidi tubadilike na pia wananchi na wadau kwa ujumla msitulaumu mana wakongwe tunajaribi kuwashirikisha ila mameneja wao ndio hawataki.
Mwisho mahojiano.
Nipehabari ilifanya pia mahojiano na msanii chipukizi na hivi ndivyo ilivyokuwa:
Nipehabari: Hivi umeshawahi kuombwa kushirikishwa na wasanii wenzako hasa wakongwe kwenye nyimbo zao?
Chipukizi: Ndio nimewahi mara kadhaa kutafutwa na wasanii wakongwe ila nimeshindwa kushirikiana nao mana meneja wagu hakutaka nifanye hivyo kulingana na mkataba niliyosaini naye.
Mwisho mahojiano.
Hivi hatuoni wenzetu waliotutangulia katika tasnia hii ya muziki mfano wamarekani ,wasanii kama lil wayne ndani miaka 3 alivyoshirikishwa na kushirikisha wasanii wenzake chipukizi na wakongwe zaidi yake katika nyimbo.Hii imemsaidia kumuongezea umaarufu na kujulikana duniani. Pia msanii kama nick minaj ambaye ametoka hivi karibuni lakini kwa sasa ameshashirikishwa kwenye nyimbo nyingi sana za wakongwe.mfano monster ya kanye waste,all I do is win(rmx )ya dj Khalid na nyingine kibao.Hii ndio inamfanya sasa hivi kuzidi na kuendelea kuwa gumzo katika vyombo vya habari kote duniani.
Wapo watasema nimetoa mifano ya nje tu,Haya kibongo bongo msanii juma nature kipindi hicho anatoka alishirikishwa au kushirikisha watu wasanii wengi sana kabla ya kutoa album yake ya pili iliyokwenda kwa jina la ugali.Hata baada ya hapo aliendelea kushirikiana na wasanii wenge katika nyimbo nyingi ambazo zinamfanya mpaka leo ndio awe msanii pekee mwenye shangwe kubwa kuliko wote kila apandapo kwa jukwaa.
Hivi nyie mnaojiita mameja wasanii chipukizi mnawatumia tu au mnataka wapate mafanikio?
No comments:
Post a Comment