TFF imemsimamisha kazi
FROLINAN KAIJAGE
Shirikisho la soka nchini TFF limemsimamisha kazi msemaji wa Shirikisho hilo TFF FROLINAN KAIJAGE baada ya kushindwa kupiga nyimbo za taifa wakati wa mchezo wa kufuzu fainali za mataifa la Mataifa ya afrika kati ya morocco na Taifa Stars ya Tanzania
Rais wa TFF RODGER TENGA amesema kwa kushirikiana na wizara ya Habari Utamadunia na Michezo wanaunda kamati ambayo itachunguza chanzo cha tatizo hilo huku KAIJAGE akiwa nje mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.
Lakini katika hatua nyingine RODGER TENGA amesema ndani ya mwezi mmoja TFF inatarajia kutangaza nafasi mbili ya katibu wa TFF na msemaji wa TFF ili kuziba nafasi hizo haraka iwezekanavyo.
Janejohn5.blogspot.com

No comments:
Post a Comment