Chadema kuburuzwa mahakamani Tarime
MSIMAMIZI wa uchaguzi Jimbo la Tarime, Fidelis Lumato ametishia kuwaburuza mahakamani waliokuwa mawakala wa Chama cha CHADEMA,kwa kughushi matokeo endapo aliyekuwa mgombea wa ubunge wa chama hicho, Mwita Waitara atafungua kesi kupinga matokeo hayo.Lumato ametoa kauli hiyo jana,Tarime, ikiwa ni siku chache baada mgombea huyo , kuwaambia wandishi wa habari kuwa amebadili uamzi wa kutaka kujiua baada ya kuibiwa kura sasa anakusudia kwenda mahamakani kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM.
Kufuatia kauli hiyo jana msimizi wa uchaguzi huo, aliitisha mkutano na waandishi wa habari akaeleza kusikitishwa jinsi mawakala wa Chadema walivyo ‘chakachua’ nakala za matokeo hayo kwa lengo la kumdanganya mgombea wao kuwa ameshinda bila kujua kuwa matokeo hayo ni tafauti na nakala halisi za tume ya uchaguzi.
“Tunajua kuwa viongozi wa Chadema wapo makini hatuwezi kuwaibia kura mbona kuna mgombea wao kata ya Bumera yupo mahabusu lakini tulimpatia haki yake ametangazwa kuwa mshindi, inakuwaje tumwibie mgombea ubunge aliyekuwepo…tunajua kuwa mawakala ambao sio waaminifu ambao walibadilisha matokeo kwa lengo la kuwadanganya wagombea wao kuwa wameshinda”alisema Lumato
Lumato alisema kuwa endapo mgombea huyo wa Chadema atatumia nakala zinazoonyesha kuwa alishinda kwenda kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo hayo wakati nakala hizo ni za kughushi atawafunguliwa kesi ya jinai mawakala wote waliohusika na mchezo huo.
“Kwasasa tunamsubiri aende mahakamani kama alivyodai, akiwasilisha tu zile nakala kama vielelezo ambazo tunaamini zimeghushiwa tutazitumia na sisi kama ushahidi kuwashitaki mawakala wote waliohusika kubadilisha matokeo hayo”alisema Lumato
Aidha Msimamizi huyo alishangazwa na matokeo ya mawakala wa Chadema kutafautiana na mawakala wa vyama vingine,alitaja baadhi ya vituo ambavyo wameona nakala zake zimebadilishwa tafauti na matokeo halali kuwa ni Turwa, Kata ya Kibasuka,Matongo na kata ya Nyarero.
“tunajua kughushi ni kosa la jinai lakini tunawasubiri wapeleke nakala hizo mahakamani ili tuzitumie kama ushahidi kuwafungulia mashtaka mawakala hao,kwa kughushi matokeo jambo ambalo lingeweza kuleta maafa endapo wafuasi wa CHADEMA wangeyatumia kudai ushindi”alisema Lumato
Wakati msimamiz huyo akijibu madai hayo, Waitara anatarajia kutinga ndani ya siku 14 ili kupinga matokeo hayo kwa madai kuwa anaushahidi kutoka kwa mawakala wa chama chake ukionyesha kuwa kura zilizotangazwa ni tofauti na kura alizopata kwenye vituo jambo analoamini kuwa aliibiwa ushindi.
Kauli hiyo aliitoa katika mkutano wake na wandishi wa habari ambapo alisema kuwa licha ya kuwa amenyang’angwa ushindi wake kwa nguvu hatokubaliana na matokeo hayo hadi pale atakapo hakikisha kuwa haki inatendeka na ikiwezekana kurudiwa kwa uchaguzi katika Jimbo hilo kw3ani ana dai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki jimboni hapo.
Mwikwabe alisema kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakipo Tarime kwa bahati mbaya ni chama kinachopendwa na wapenda amani wa Tarime hivyo mapambano yataendelea zaidi na hata akipoteza maisha huku akitolea mfano alivyofariki Chacha Wangwe alie kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime kabla ya kufariki dunia kwa ajari ya gari na kudai kuwa , Mapambano yataendelea kuwepo.
Alisisitiza kuwa pamoja na yeye na watu wake kuwekewa mazingira magumu kwa kupingwa mabomu ovyo na wengine kuendelea kusota mahabusu tangu tarehe 25mwezi jana yeye hakuwa tayari na hakutaka damu za wana Tarime zimwagike kwajili ya ushindi ,hivyo aliamua kukakaa kimya huku akijipanga kwaajili ya kutafuta haki yake katika vyombo vya dola.
Aidha alisema kuwa utaratibu wa kudai haki kisheria utaendelea na hatimaye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) itashinda bila kumwaga damu na kuongeza kuwa yeye hakusaini kutokana na kwamba ushindi huo ni batiri hivyo ameamua kutafuta wakili atakaye msaidia kupata haki yake mahakamani.
“Nilikuwa nasubili hasira ipungue ili niweze kufanya maamuzi sahihi sasa nimeamua niende mahakamani baada ya kuwa na ushahidi wa kutosha sambamba na vielelezo, na hata hivyo makosa mengi yaliyojitokeza katika uchsguzi nililalamika kwa msimamizi mkuu wa uchaguzi Fidelis Lumato lakini sikusikilizwa.”alisema.
Akiendelea kuzungumza alisema kuwa pamoja na upolaji huo wa kinguvunguvu bado wananchi wa Jimbo la Tarime na wapenzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)hawajaondoa imani na chama chao n wanacho taka ni haki kutendeka na sii mabavu iliamani iweze kuwepo katika Jimbo hilo.
Hata hivyo Bw. Waitara alichambua baadhi ya sehemu ambazo alikuwa anaongoza kwa kura lakini matokea yakitangazwa yanakuwa tofauiti mfano Magena kura za CCM ubunge zilikuwa 46 na za CHADEMA zilikuwa 105 baada ya kutangazwa CCM ilikuwa 112 ambapo CHADEMA zilipungua na kubaki 95 pia kituo cha Rebu CCM ilipata kura 34 zikatangazwa 274 Siraari 4 zikatangazwa 28.
Bw. Waitara alitoa malalala miko kwa baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Tarime na kudai kuwa walijihusisha katika kusimamia katika vituoa vya kupigia kura na hali hiyo kusababisha matokeo yake kuchakachuliwa na mgombea Ubunge kupitia Chama cha mapinduzi kutangazwa kuwa mshindi.
Hatahivyo Nyambari Chacha Nyangine aliekuwa mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM)alitangazwa kuwa mshindi katika kinyanganyiro hicho kwa kura 28,064 huku alie kuwa mgombe kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuambulia kura 27,334, NCCR MAGEUZI kura 7811 na alie kuwa mgombe kwa tiketi ya CUF Charles Mwera Nyanguru kuambulia kura 7368.
Habari kwa ihsani ya Mobini Sarya
Tarime
No comments:
Post a Comment