Tuesday, November 16, 2010

MIZENGO KAYANZA PINDA NDIYE WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Haikuwa rahisi kufikia hapo baada ya baadhi ya wabunge walikataa kupitishwa jina la mheshimiwa pinda kuwa waziri mkuu baada ya kuteuliwa na raisi wa muungano wa Tanzania mheshimiwa jakaya mrisho kikwete.Utaratibu uliofuata ni kupiga kura kwa mbunge mmoja mmoja ili kila mmoja kuchagua kama mheshimiwa pinda  anafaa au laa.

Kura zilizopigwa zilikuwa 328, kura zilizoharibika  ni 2,kura za wale waliosema hapana ni 49 na kura zilizompitisha mheshimiwa pinda ni 277.Baada ya kutangaza matkeo hayo mheshimiwa spika akamtangaza mheshimiwa pinda kuwa waziri mkuu aliyepitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment