Saturday, December 11, 2010

Ivory coast walivyoingia fainali hapo jana
Jana wakati naenda uwanjani mida ya saa 8 mchana purukushani za watu kutafuta tiketi ili kuingia uwanjani zilikuwa zimepamba moto.Hii pia ni kwa sababu walanguzi wa Tiketi walikuwa wengi sana yani tiketi ya shilingi 1000 unauziwa sh 2000 mpaka 3000.

Kama kawaida vijana wameshalanguliwa tiketi na ndio wanaelekea geti la kuingilia.

Kwa siku mbili hizi yani mechi ya robo na nusu finali mageti ya kuingilia ni ya mbele tu mengine yote yalikuwa hayafanyikazi.

Wamachinga walikuwa wengi baadhi walikuwa wanauza jezi za timu ya kilimanjaro stars kama huyu kaka anavyoonekena pichani

Sio wanaume tu wanaopenda mpira na hasa timu yao ya taifa hata wakina dada walikuwa wengi.Na pia sio tu kwamba lazima waje na mtu hata peke yao wanaweza kuja.Hongera sana dada inagawa jina lako sikulipata

Nilikuta mazoezi ya Timu za ivory coast na Ethiopia yakiendelea kama uonavyo



Na hapa ndio wanaingia uwanjani

Baada ya nyimbo zao za taifa mpira ulianza kwa mashambulizi na mpira mzuri wa pasi fupi na kuonana kutoka kwa Ethiopia.Kusema kweli kama mpira ungekuwa pasi basi jana Ethipia walitakiwa kushinda lakini ndio hivyo walikuwa hawana washambuliaji mahiri na viungo wa kupenya ngome ya ivory coast


kama kawaida watu wa fujo huwa hawakosekani,jamaa mwenye kipara alikuwa anasindikizwa na mapolisi baada ya kufanya fujo


Ndio kilimanjaro stars na uganda walipoingia kufanya mazoezi wakati mechi ya kwanza ikifikia ukingoni.
Ivory coast walishinda dakika za mwisho goli 1

No comments:

Post a Comment