Jana nje ya uwanja mambo yalikuwa kama hivi ili kulinda usalama wa raia na kuwaadhibu wale watukutu.
Nadhani unaweza kujionea mwenyewe jinsi watu walivyokuwa wengi na hapa ni wakati ambapo mechi ya kilimanjaro stars imeshaanza.Tiketi zilikuwa hazipatikani kabisa kwa habari nilizopata kuanzia sa 3 asubuhi tiketi ya Tsh 1000 ilikuwa inauzwa Tsh 3000.Na muda ulivyokuwa unasogea mida ya saa 9 alaasiri ilikuwa inauzwa mpaka Tsh 10000.
Baadhi ya matukio katika picha wakati mechi ya kilimanjaro stars na Ivory coast ikiendelea.
Muda ambapo refa aliamuru ipigwa penalti baada ya kufanyika madhambi kwenye lango la timu ya ivory coast.
Muda wa mapumziko Viongozi mbalimbali walikuwa wanabadilishana mawazo,kama unavyoona katika picha ni Mohammedi dewji na viongozi wengine.
Wachezaji wakiingia uwanjani tiali kwa kipindi cha pili kuanza
wakati kipindi cha pili dakika zinaishia ndipo mwali alipoletwa uwanjani mana mahari imeshatolewa tiali
Mashabiki wa kilimanjaro stars wakishangilia kwa furaha huku wakiomba muda uishe haraka baada ya kutangazwa dakika 3 za majeruhi zimeongezwa.
Na mpira umekwisha
Vingozi wakipongezana kama unavyowaona pichani

No comments:
Post a Comment