Samahani kwa usumbufu
Wana nipehabari kwanza natanguliza samahani kwa usumbufu uliojitokeza kwa kuto kuwa hewani kwa muda wote wa mwisho wa mwaka.Kwa maneno mengine tumeumaliza mwaka vibaya sana maana kulikuwa na tatizo katika blog ambalo halikujulikana mapema na bado tunalifanyia kazi ingawa kwa sasa kiasi fulani limepungua.Ilikuwa tunashindwa kuweka habari mpya na kupreview kile tunachoweka kabla hakija kufikia wewe msomaji mana hilo ni jambo muhimu kwetu.Pia katika upande wa wasomaji walikuwa wanalalamika kutoweza kufungua blog kabisa ambapo ilikuwa kweli.Naomba tusameheane na tuendelee kupeleka gurudumu la blogs mbele.
Baada ya kusema hayo namuomba mungu atujaalie mwaka 2011 uwe ni wenye maendeleo kwetu sote na atulaalie afya njema na kumjua yeye zaidi na zaidi mana bila yeye tusingevuka mwaka.Wangapi tumewaacha 2010 na ambao walitaka kuendelea kuishi zaidi zaidi.
No comments:
Post a Comment