Thursday, July 30, 2009



CHOKORAA ANUSA JELAA,

Mwanamuziki wa bendi ya African Stars ‘Twanga pepeta’ Khalid Chuma “Chokoraa”, amefikishwa jana kwenye Mahakama ya Mwanzo Magomeni akikabiliwa na shtaka la kumtukana matusi ya nguoni askari wa usalama barabarani. 


Mwanamuziki huyo anadaiwa kumtukana trafiki wa kike Janeth baada ya kutokea mabishano kati yao. 

Imedaiwa kuwa mwanamuziki huyo alikuwa anashindwa kuendesha gari lililokuwa kwenye foleni, baada ya kuamriwa kufanya hivyo na askari na badala ya kuendesha akamtukana. 

Ilidai kuwa Julai 27 mwaka huu, saa 12 jioni huko Magomeni Mikumi, mshtakiwa alimtukana afande Janeth matusi ya nguoni. 

Imedaiwa kuwa siku hiyo, askari huyo alikuwa anaruhusu magari kwenye foleni, lakini gari la mshtakiwa lilikuwa limesimama badala ya kutembea ndipo alipomfuata na kumuuliza kulikoni. 

Pia, imedaiwa kuwa alimuuliza anakwenda upande gani, kama wa kushoto basi awashe taa zinazoonyesha kuwa anakwenda huko, au aweke gari lake pembeni ili wenzake walio nyuma wapite, lakini mshtakiwa bado aliendelea kusimama. 

Baada ya hapo, ikadaiwa kuwa askari huyo alimuuliza amejifunza wapi udereva, anajifunza au amechukua gari la ndugu yake, ndipo mshtakiwa alipojibu kwa kumtolea matusi. 

Mshtakiwa amekana shtaka hilo na alikuwa bado hajadhaminiwa, lakini baadhi ya wanamuziki wa bendi hiyo, ndugu, jamaa na marafiki wakiongozwa na Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka, walikuwa akifanya harakati za kumuwekea dhamana kortini hapo.

No comments:

Post a Comment