Monday, July 27, 2009

Miss Temeke Kujulikana Jumamosi

Shindano la kumfuta kisura wa wilaya ya Temeke ambaye ataiwakilisha wilaya hiyo kwenye mashindano ya Kitafaifa ya Miss Tanzania 2009 linatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii katika ukumbi wa TCC Chang’ombe. 


Akiongea na Nipehabari mratibu wa shindano hilo toka kampuni ya BMP Benny Kisaka alisema mipango yote tayari kwa ajili ya mtanange huo. 

“Kama tulivyowaarifu shindano lenyenyewe litakuwa siku ya tarehe 31 mwezi huu yani Jumamosi ijayo ambapo warembo watapanda jukwaani kumtafuta mwakilishi wa Miss Kinondoni kuelekea Miss Tanzania hapo baadaye, zaidi ya shindano hilo pia kutakuwa na burudani toka kwa Marlaw, Twanga Pepeta na burudani nyingine nyingi tu” alisema Benny 

Temeke mojawapo ya wilaya ambazo zimewahi kufanya vizuri katika mashindano hayo itataka kujiwekea mwiko wa kusubmbuliwa na Kinondoni ambao ndio wababe wa mashindano hayo kwa kupeleka mwakilishi mwenye sifa na vigezo. 

Mazoezi ya washiriki yanaendelea chini ya mwalimu wao Lona Swai, Nyamwela na wengine. 

Kiingilio ni Tshs 50,000/- kwa VIP, wadhamini wa Reds Miss Temeke mwaka huu ni Mariedo Boutique, Valley Springs, Ally Rhemtullah, Screen Masters, 88.4 Clouds FM na wengine.

No comments:

Post a Comment