Monday, July 27, 2009


Unakumbuka toka Pwaa ya kwanza kabisa iliyobamba ipasavyo katika anga za Bongo Fleva? 

Ikaja Pwaa Part ngoma iliyosimamiwa na Mtu mzima Lucci ambapo ilimpeleka CP katika Level nyingine kabisa, Level za kimataifa, kwani kiukweli ukiangalia au kusikiliza ngoma ya Pwaa Part2 utakubali ya kuwa CP alifanya kazi ya ziada kuanzia utunzi wake mpaka shooting ya Video yake ilikuwa katika “another Level”, ili kuwapa wapenzi na washabiki wake mautamu zaidi na kuonyesha nini amekusudia mchizi muda si mrefu ataachia songi lake la Pwaa Part3. 

Bila kuweka kazi ni nani na nani watakaokuwa wamesimama kwenye ngoma hiyo, CP wakati anaongea na Nipehabari alisema ya kuwa huo ni mwendelezo wa ngoma yake hiyo ambapo kwa madai yake mwenyewe mchizi amesema anatarajia kuifanya tofauti zaidi, na habari za ndani zinasema kuna Pwaa kibao zinakuja, sasa mpenzi na mshabiki wa CP na muziki wa Bongo Fleva kwa ujumla kaeni mkao wa kula kumsikiliza na kumuona jamaa ubunifu zaidi na zaidi.

No comments:

Post a Comment