Tuesday, March 2, 2010


Wadu hii ni kwa ajili ya wale wezi wa wanao endelea kuiba pesa za wateja wa G4S nchini kenya G4S imesema !
..eeeh...wewe hapo kwa computer…...
ati unajidai wewe ni sonko eeehhh!!!........
Na je?, huyo jamaa wa hapo kwenu.....unajua yeye hufanya G4S ??....
Kuna njia moja tu ya kumaliza ufukara,
Andikwa G4S.....
ponyoka na kijisanduku cha pesa.....!!!!!!!!!!
Chanuka! Epuka ufukara.





Beenie Man - "Swagga Mi Flow" Video 2010









Wiki iliyopita Kaka Sunday Shomari alinitaarifu juu ya mkutano / kongamano kuhusu CLEAN WATER FOR AFRICA lilioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Harambee International Development na Constituency for Africa ambalo lilifanyika Jumamosi na kuzungumzia meengi kuhusu ufanikishaji wa kusambaza maji safi na salama barani Afrika. Nilibahatika kuhudhuria. Kati ya waliohudhuria kongamano hilo ni Dr Julius Garvey ambaye ni mtoto wa mwisho / kitindamimba wa mpigania haki za watu weusi Hayati Marcus Garvey ambaye pia alianzisha Universal Negro Improvement Association mwaka 1914. Katika kongamano hilo la kwanza kufanyika na ambalo linataraji kuwa la kila mwaka, yalizungumzwa mengi na mwisho wake nikabahatika kupata nafasi ya kuzungumza na Dr Garvey. Nilimuuliza kuhusu

UKOLONI MAMBOLEO UNAOENDESHWA NA WAZALENDO JUU YA WAAFRIKA WENZAO NA KUBWA ALILOSEMA NI KUWA
VIONGOZI WENGI WA AFRIKA WANA FIKRA ZA KIKOLONI. TAZAMA SWALI NA JIBU LAKE HAPA CHINI










Wachezaji nane wa timu ya soka ya taifa, Taifa Stars na kikosi kamili cha Uganda, The Cranes, jana wamekwama kuelekea jijini Mwanza kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza ambayo yalisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha jijini humo.

Tatizo hilo lilitokana na ndege ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) iliyokuwa inatoka jijini Dar es Salaam kupata ajali na hivyo kupelekea ndege nyingine kushindwa kutua wala kuruka kutoka katika uwanja huo jana.

Akizungumza jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela, alisema kwamba kutokana na tatizo hilo, wachezaji hao wa Stars ambao wanaichezea klabu ya Yanga walilazimika kurejea nyumbani na hivyo safari yao inatarajiwa kufanyika leo.

Mwakalebela alisema kuwa tatizo hilo liliwakumba pia The Cranes ambao tayari walikuwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe nchini Uganda na kulazimika kusitisha safari hiyo.

Alisema kwamba The Cranes pamoja na wachezaji hao wa Stars wanawatajiwa kuwasili Mwanza leo asubuhi tayari kujiandaa na mchezo huo uliopangwa kufanyika kesho kwenye uwanja wa CCM, Kirumba.

Aliwataja nyota hao waliokwama kuwa ni pamoja na Mrisho Ngassa, Jerryson Tegete, Abdi Kassim, Nadir Haroub 'Cannavaro', Nurdin Bakari, Kigi Makasi na Shadrack Nsajigwa, ambao walirejea jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambako klabu yao ilitolewa na Saint Eloi Lupopo katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kufungwa jumla ya magoli 4-2.

"Tuna imani mambo yatakwenda vizuri na timu zote zitakuwa jijini Mwanza kabla ya kesho mchana ili kuweza kuchuana hapo Jumatano," aliongeza Mwakalebela.

Chanzo chetu kilichokuwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, kilisema kwamba wachezaji hao walikaa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa nne na kwamba ilipofika saa 7:00 mchana waliambiwa kuwa safari imeshindikana.

Kutokana na tatizo hilo, The Cranes nao walilazimika kurejea jijini Kampala, Uganda kuendelea na mazoezi mpaka pale watakapofahamishwa kuwepo kwa safari hiyo.

Alisema kwamba mechi hiyo imepangwa kufanyika kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo viingilio ni Sh. 5,000 kwa eneo la mzunguko na viti maalumu ni Sh. 15,000.






Leo wadau ni siku ya kuzaliwa king of Bongo Crunk cpwaa hii picha wadau imetengenezwa na vijana wajulikanao kwajina la Crunk Boys wakitoa big up kwa cpwaa, twakutakia kila laheri king .





JAMES anapenda kuwakaribisha wote ndani ya SEE WEAR ambako kumewasili mali mpya aka 'pamba'. Pamba za SEE WEAR ni za high quality kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya kila mtu. Fika SEE WEAR ukajionee mwenyewe. Kwa wale walio mbali na SEE WEAR (NAPOLI) msisite kuwasiliana nasi kupitia E-mail ya blog hii.Gharama za utumaji pamba zitalipwa na SEE WEAR: -SEE WEAR iko mtaa wa: VIA STAFFETTA No.127 ,LAGO PATRIA GIUGLIANO NAPOLI-ITALY.(Picha na Gfamily)








Wapenzi wa jinsia moja wavuruga ibada, Uholanzi
Nchini Uholanzi, mamia ya wanaharakati wanaounga mkono ndoa za mapenzi ya jinsia moja walitoka nje wakati misa ikiendelea katika kanisa moja la katoliki ambapo walikuwa wamekusanyika kupinga sera ya kanisa hilo juu ya uhusiano wa aina hiyo.

Walivuruga misa kwa nyimbo na kumzomea kasisi aliyekataa kumpa sakramenti mmoja wa waumini hao aliyetangaza wazi kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Uholanzi ni taifa la kwanza bara Uropa kuidhinisha ndoa za aina hiyo katika mwaka wa 2001.

Hata hivyo kanisa Katoliki nchini humo limeendelea kupinga ndoa hizo.

No comments:

Post a Comment