Sunday, March 7, 2010

ELEPHANT MAN NEW VIDEO 2010 PARTY UP IN HERE .







Ombaomba sasa wacharuka kuhusu manyoya


Ule uvumi wa walemavu wanaoombaomba jijini kuwasababishia madhara watoa msaada umewatokea puani kituo maarufu cha Redio nchini Clouds FM, baada ya kutakiwa kuomba radhi na kubadilisha usemi wao hadi Alhamisi vinginevyo kuswekwa rumande.

Wakizungumza mbele ya vyombo vya habari leo asubuhi katika Ukumbi wa Habari Maelezo Dar es Salaam, wawakilishi wa kikundi cha walemavu jijini wamesema kitendo cha mama aliyempa ombaomba fedha mkono ukaota manyoya Selander Bridge ni uzushi mtupu kwa kuwa hakuna uthibitisho.

Mmoja wa wawakilishi hao Enyimba Robert mkazi wa Temeke amesema kuwa suala hilo lilitiwa chumvi na vyombo vya habari na hakuna ukweli ndani yake, huku wakiwasakama vilivyo Clouds kwamba waliongea sana kuhusu uvumi huu.

Bwana Enyimba ambaye ni baba wa watoto wanne amewataka Clouds wathibitishe kauli hiyo mara moja kwani imewaletea madhara makubwa ikiwemo kukataliwa katika jamii.

Amesema licha ya kupata kejeli kutoka sehemu mbalimbali, Enyimba binafsi amepewa notisi na mwenye nyumba wake Said Hamis, ikimtaka kuondoka kwa madai kuwa wapangaji wenzie wanaogopa kupata manyoya.

Naye Neema R. Masagila mkazi wa Temeke kutoka mjini Morogoro, amesema hadi kufikia Alhamisi ya wiki hii Clouds wanatakiwa wawe wamethibitisha taarifa hiyo au kutangaza upya kufuta kauli hiyo vinginevyo watapelekwa mahakamani.

‘Tunakataliwa kila mahali sasa, majumbani, kwenye daladala, migahawani, na pia kodi zetu za nyumba zimepandishwa kwa sababu ya usemi huu’ ameeleza Masagila

Amesema kwa wakati huu wanaogopa sana suala hili lisije likawa kama la ndugu zetu Albino na hivyo kuitaka jamii kubadili mtazamo wao.

‘kwa ujumla sisi hatuna cha kuwaeleza Watanzania, ila tunataka Clouds wawaambie wananchi mioyo yao huyo mama yuko wapi, na hayo manyoya yako wapi na gari walilosema mbona halipo?’ ameuliza mama huyo

Aidha Bi. Masagila anayeombaomba katika maeneo ya Nyerere Road,naye amekiri kupewa notisi ya kuondoka nyumba aliyopanga, na kukitaka chombo hicho cha habari na wengine waliotangaza uvumi huo kwenda pale Selander Bridge kuthibitisha suala hilo kwa wananchi.




Soko la kahawa Duniani lakua wakulima washauriwa kuongeza bidii kwenye uzalishaji wa kahawa.


Akibainisha hayo kwa Wanahabari hii leo, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa nchini Pius Ngeze amesema kufuatia mkutano wa Shirika la Kahawa Duniani uliofanyika tarehe 26-28 Feb. mwaka huu nchini Guatemala, uzalishaji wa zao hilo unakumbwa na vikwazo vingi vinavyopunguza uzalishaji. Mkutano huo uliolenga kutathmini maendeleo ya uzalishaji na mwenendo wa soko la zao hilo, umebainisha kasoro zilizopo kuwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, kupanda kwa gharama za uzalishaji, kuwepo biashara ya magendo isiyomnufaisha mkulima pamoja na bei ndogo sokoni miongoni mwa matatizo mengine. Bwana Ngeze ameeleza kuwa kikao hicho kiliazimia kuweka sera za masoko kulinda zao hilo, kuhamasisha unywaji, kuweka mikakati ya kudhibiti changamoto zilizopo na kujipanga zaidi kuongeza uzalishaji. Kadhalika Mwenyekiti wa Bodi hiyo nchini yenye makao yake makuu mkoani Kilimanjaro ameeleza kuwa kufuatia taarifa za kikao hicho, nchi watumiaji zilidai kuhitaji zaidi kahawa na kutaka uzalishaji uongezwe hasa katika masoko mapya ya India na Urusi pia China iliyotajwa kama soko ambalo bado halijafikiwa. Aidha kiongozi huyo amewataka Watanzania kujipanga upya kuliimarisha zao hilo katika wakati ambao Bodi inafanya jitihada kudhibiti biashara haramu ya magendo inayowaumiza wakulima. Pia amewahimiza wananchi kupenda kunywa kahawa kama hatua mojawapo ya kuliinua zao hili na kusema kwa sasa ni 5% ya wananchi wanaokunywa kahawa, wakati Brazil ni 17% huku bei yake kwa sasa ikitajwa kuwa senti 120 za dola kwa ratili.









ANTI-SMOKING ADVICE AT FUNERAL


A life-long smoker has had his dying wish honoured when he had the words "Smoking Killed Me" placed on signs in his hearse. Albert Whittamore, known as Dick, died last month aged 85 after suffering for years from emphysema, a progressive lung condition he blamed on his habit. He wanted the ill-effects of his smoking to act as a warning to others and dictated in his will that the signs be placed inside his hearse as it passed through his home town of Dover in Kent. One of the signs was also placed at Mr Whittamore's graveside, according to his wishes. Paul Sullivan, of Sullivan & Son funeral directors, said: "Although he had reached the age of 85, he had been suffering for a while and wanted to do his bit to warn others about smoking. "He specified that that's what he wanted in his will. We gave it some thought but after a while we decided that that's what he had requested." Mr Whittamore, who ran a small printing business in a shop below his home, was forced to use a motorised wheelchair in his later years as his health faltered. A spokesman for the stop smoking charity Quit said: "We understand Dick had emphysema, which is a lung condition caused by smoking which results in people struggling for breath. "Dick is sending out a strong message to smokers as he doesn't want others to suffer. "Smokers can ring Quitline, 0800 00 22 00, to get advice on how to quit and to pay tribute to Dick."





Patrick Newman msanii wa Kibongo anayefanya muziki wa Gospel ambaye makazi yake ni pale Seattle, Washington nchini Marekani. Yeye si mgeni katika anga za muziki. Kwa muda sasa amekuwa akifanya kazi zake nchini Marekani.









Askofu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF), Zacharia Kakobe kwa mara nyingine tena, amekuwa ngangari kwa kuitunishia Serikali misuli kupinga mradi wa umeme wa msongo mkubwa wa kilo voti 132 wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) usipitishwe mbele ya kanisa.




HIP HOP STAR LIL WAYNE A.K.A WEEZY HISASA JAMAA YUPO JELA KWA KOSA LA KUKUTWA NA SILAHA NDANI. JAMAA KAENDA JELA MWAKA MMOJA MASHABIKI WA LIL WAYNE BONGO MNAONAJE TUKIO HILI !












No comments:

Post a Comment