JUMUIYA YA WANAFUNZI WAKATOLIKI WA IFM
Ndugu wapendwa tunapenda kuwapa taarifa juu ya matendo ya huruma yaliyofanyika jumamosi tarehe 19 desemba 2009.
Wapendwa katika kristo jumuiya ya wanafunzi wakatoliki IFM imejiwekea utaratibu wa kuwatembelea na kawapa zawadi wagonjwa,wafungwa,watoto yatima na wenye matatizo na wanaoishimkwenye mazingira magumu mara moja kwa muhula wa masomo.Katika kusheherekea sikukuu ya christmas na mwaka mpya jumuiya ilipanga kuvitembelea vituo viwili vya watoto yatima.kituop kinachoitwa songambele pamoja(SOMBEPA) kilichopo kigamboni na kituo cha watoto yatima kinachosimamiwa na serikali kilichopo kurasini.Haya ni baadhi ya matukio.
Baadhi ya wanachama wa jumuiya ya wanafunzi wakatoliki wa IFM wakiongea na watoto yatima kituo cha kurasini.
Mtoto yatima akilishwa keki na mwanafunzi wa IFM.Aliyevaa ushungi ni mama mlezi wa kituo.
Brother akimsaida mtoto ili aweze kunywa juisi
No comments:
Post a Comment