Friday, May 21, 2010

KATUNI ZA BROTHER FEDE
Kwa kupata katuni zaidi ingia kwenye hii blog
www.artsfede.blogspot.com

NGASSA HUYO KUELEKEA AZAM F.C

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa sasa yupo huru kwenda kuichezea timu ya Azam FC msimu ujao, baada ya kikao cha viongozi wa pande zote mbili kukubaliana mambo mbalimbali.
Kikao cha kujadili ofa ya mchezaji huyo kilianza juzi na jana mchana, kilimalizika ambapo Azam FC, walianza utaratibu wa kuwalipa Yanga dola za Marekani milioni 40 (zaidi ya sh.milioni 50 za Tanzania).
Habari kutoka ndani ya kikao hicho, zinadai kuwa, kikubwa kilichokuwa kinajadiliwa katika kikao hicho ni dau la mchezaji huyo, ambapo walikubaliana kutoa kiasi hicho cha fedha na kutoa baraka kwa mchezaji huyo kutua Azam.
"Sasa hivi (jana) tunakwenda kuchukua kiasi hicho cha fedha ili tumalizane na wenzetu wa Yanga, kikao kilikuwa cha amani na tulifuata taratibu zote zinazotakiwa," kilidai chanzo hicho cha Azam kutoka ndani ya kikao hicho.

Chanzo hicho kilidai kuwa, baada ya kukamilisha mipango ya kumnasa Ngassa, sasa wanaendelea na mipango mingine ya kutafuta wachezaji wengine kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao msimu ujao.
Kilidai kuwa, msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara wamepanga kunyakua ubingwa wa Bara, ili nao waweze kushiriki michuano ya kimataifa. Pia, klabu ya Yanga inaweza kumpoteza beki wake mahiri Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye naye anadaiwa kutaka kuhamia klabu hiyo ya Azam.

No comments:

Post a Comment