Tuesday, July 20, 2010

Tottenham timu ya kwanza kukataa VUVUZELA

Tottenham imekuwa timu ya kwanza katika ligi kuu ya Barclays kukataa matumizi ya vuvuzela katika uwanja wao wa White Hart Lane  wakati wa mechi zitakazo anza mwezi wa nane.

Uamuzi huo umetolewa baada ya mazungumzo na polisi pamoja na mamlaka ya mji huo.Spurs wamesema kuwa makelele yanayotokana na vuvuzela yanaweza kusababisha hatari ambazo zinaweza kuepukika kwa mfano,watu kushindwa kusikia matangazo yatakayokuwa yanaashiria  hatari fulani uwanjani.
Pia makelele yatakuwa yanawasumbua wakazi wanaozunguka uwanja huo.  

No comments:

Post a Comment