DC na DED wagombea ruzuku BUNDA
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bunda imeingia katika mgogoro mkubwa wa kugombea ruzuku na mamlaka ya mji mdogo wa Bunda baada ya mkurugenzi wa Wilaya hiyo kudaiwa kugomea ruzuku ya mji huo.
Kufuatia hatua hiyo mamlaka ya mji huo imemshitaki mkurugenzi huyo Cyprian Oyeir kwa mkuu wa wilaya hiyo Francins Isac ili aweze kutatua mgogoro huo.
Baraza hilo ambalo linaundwa na wenyeviti wa vitongozi 38 jana walimshambulia mkurenzi huyo wakimtuhumu kuwa kikwazo cha mji huo baada ya kugoma kuwapatia Mil.82 zinazotolewa na serikali kila Mwaka kama ruzuku ya ustawishaji mji mdogo.
“hapa lazima tuache utakatifu nyuma tuhakikishe tunapambana hadi haki ipatikane ikishindikana kwa mkuu wa wilaya tutamfikisha kwa Mkuun wa Mkoa ambaye ni Mwakilishi wa Waziri” alisema Mgendi Makanyaga ambaye ni M,wenyekiti wa Kitongoji cha manyamanyama shuleni.
Aidha Mwenyekiti wa mamlaka ya mji huo Pastory Ncheye alieleza baraza la mji huo ambalo lilikutana jana kwa ajili ya kujadili tatizo hilo kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Francis Isack amejaribu kumuita mkurungenzi huyo zaidi ya mara tatu ili watatue mgogoro huo lakini imeshindikana.
Baada ya kutolewa majibu hayo wajumbe wa baraza hilo walicharuka na kumtaka mwenyekiti huyo ambaye pia ni Meya wa Mji aende kumwita DC ili aje kueleza mwenyewe baraza hilo kwanini mkurugenzi anakatalia ruzuku yao hali ambayo inawafanya uendashaji kuwa mgumu huku wakiambulia Posho ya 20,000 badala ya 40,000.
Hata hivyo baada ya Meya kumfuata Mkuu wa Wilaya ofisini kwake, ali mkuta akiendelea na kikao cha kamati ya siasa ambapo alijibiwa kuwa bado anasubiri majibu ya Mkurungezi.
“wajumbe mlinituma kwa mkuu wa wilaya ili aje kuwaeleza alipofikia na mkurungenzi lakini ameniambia hawezi kuja na majibu ya blaa blaaaa anamsubiri mkurugenzi amlitee majibu wakati huo anaanda majibu kamili kulingana na hatua alizochukua kama DC”alisema Ncheye
Baada ya majibu hayo wajumbe wao walilamika huku wengine wakidai kuwa wamekuwa wakiambulia posho ndogo ya shilingi 20000 wakati walisatahili kulipwa 40000 lakini mkurugenzi amekatalia mapato yao ya Mwaka Mzima.
Ofisa Mtendaji wa mji huo (TEO)William Mabanga alisema kuwa serikali inapatia mji huo shilingi Milioni 82 kwa mwaka sawa na Milioni 6.8 kila mwezi ambazo hupitia ofisi ya DED.
lakini katika kipindi cha Mwaka wote uliopita wameambulia milioni 22 tu huku DED akidai kuwa mamlaka ya mji huo haina Kasma hazina.
Aidha Mabaga alisema kuwa baadhi ya vyanzo vya mapato walivyokuwa wanategemea vimebinafsishwa kwa watu binafsi na mkurugenzi amekuwa akikataa kuwapa Milioni 8 kila mwezi ambazo aliingia mkataba wa kisheria na wakandarasi hao kwasababu kiutaratibu yeye ndiye anbapaswa kusainimakubaliano yoyote.
Akifunga kikao hicho Mwenyekiti Ncheye alisema kuwa wanampa wiki moja kuanzia sasa mkurungezi huyo ili waone kama hatawapatia ruzuku hiyo watafikiria hatua ya kumchukulia.
Mkurugenzi huyo hakuweza kupatikana ili kujibu madai hayo baada ya kudaiwa kuwa yupo nje ya ofisi kikazi.
DKT. NCHEMBA AMUAGA BALOZI WA MAREKANI NCHINI
-
Na Benny Mwaipaja, Dodoma
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa
Tanzania ina thamini mchango mkubwa wa Taifa la Marekani ka...
10 hours ago
No comments:
Post a Comment