Wednesday, August 11, 2010

WAHAMISHWA TENA
Walemavu ambao wanafanya biashara ndogo ndogo walioamishwa  mtaa wa lumumba na kwenda kuendeleza biashara zao karume karibu na ofisi za TFF sasa wametakiwa kubomoa mabanda yao na kuhamia  katika eneo la machinga complex.

Katika pita pita yangu nilikutana na mfanya biashara mmoja aliyekuwa analalamika usumbufu wanaoupata na kuhamishwa mara kwa mara.pia sehemu waliopewa ndani ya eneo lao jipya kuwa ni dogo sana mana wengi wao walikuwa wanatumia banda mmoja watu 6 na pia wana biashara kubwa ambayo haiwezi kutosha ndani ya vibanda vya wavu ambavyo wamepewa.

mfanyabiashara mwingine alisema"Hawa jamaa kweli wanatutesa na  ukiangalia kodi ya 60000 kwa mwezi ni nyingi sana mana kaeneo kenyewe ni kadogo sana "
Vibarua wakiendela na kazi ya kubomoa mabanda



Mwana mama akiendelea kuokota mabaki ya vitu vyake baada ya banada lake kubomolewa na vibarua wake.





Gari kama mnavyoliona  likiwa linasomba uchafu

No comments:

Post a Comment