HOJA TOKA KWA MDAU.
Kutokana na kutokuwa na ufumbuzi mkubwa wa nishati ya kudumu ya Umeme nchini Tanzania na kushindwa kwa uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), ningeomba Serikali kuliangalia swala zima la nishati ya umeme kwa undani zaidi, kwanini nasema hivi, ni miaka 49 tangu Tanzania tupate uhuru lakini mpaka sasa leo hii Tanzania bado inakuwa na migawo ya umeme ya mara kwa mara miaka nenda rudi na sehemu nyingine kutokuwa na umeme kabisa na kubakia kwenye giza!! Ni aibu kubwa kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Serikali ya Tanzania, Viongozi wote wa Serikali pamoja na Taifa zima,
Hauwezi kusema unataka uwe na Taifa lenye nguvu kiuchumi na kimaendeleo kama nchi haina nishati ya uhakika, utawezaje kushawishi wawekezaji waje nchini kuwekeza ktk Nyanja mbalimbali za kiuchumi na maendeleo kama kuna giza!! Hii inaonesha ni jinsi gani wahusika ktk ili jambo kutokuwa makini na kutojua kazi zao, miaka yote 49 wameshindwa kuweka mikakati thabiti ya muda mfupi na mrefu kuwezesha kulitokomeza tatizo ili??!!
Hivyo basi ningeliomba Serikali na Tanesco kuangalia yafuatayo:
Suluhisho:
A: Tungeomba Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) liweze kugawanywa eidha mara 2 au 3 ili kuzidisha ushindani pamoja na ufanisi wa Shirika kwenda kwa wateja wao ambao ni raia wa Tanzania na wengineo wasio watanzania. Mfano, Miaka ya 1990’s Uingereza iliweza kufanya reform ktk Nyanja mbali mbali ikiwemo usafiri ambapo British Rail baada ya kushindwa kufanya kazi vizuri iligawanywa ambapo matokeo yake yaliweza kuongeza ufanisi mkubwa ndani ya hiyo sekta, hivyo basi nasi tunaweza kufanya hivyo hivyo cha msingi ni kuwa waangalifu na mafisadi.
B: Serikali kuweka mtazamo na mikakati thabiti ya kuwezesha wizara ya nishati na Madini inatokomeza ili tatizo la umeme, mikakati hii iwe ya kudumu na ifanyiwe kazi kwa maana sioni sababu ya waziri wa nishati na Madini na wafanyakazi wote wa wizara ya nishati na Madini kulipwa mishahara mikubwa ambayo inatokana na kodi inayolipwa na Mtanzania na wakati huo huo kushindwa kutekeleza wajibu wa kazi zao na kushindwa kutokomeza tatizo la umeme nchini Tanzania!!
C: Serikali inatakiwa kuzidisha nguvu zake za kutafuta wawekezaji walio serious, wenye experience na wenye financial capabilities kuweza kuwekeza ktk sekta hii ya nishati na kuleta ushindani mkubwa ktk hii industry ambapo itawezesha kudumisha huduma zinazotolewa na kuwezesha kutokomeza tatizo la umeme nchini Tanzania ambapo hizi kampuni za nje zitakuja na mitazamo tofauti mbali mbali ya kuweza kupambana na ili tatizo tulilo nalo.
D: Inasemakana kwamba Tanzania tuna vyanzo vingi vya Umeme vikiwemo mito, maziwa, upepo mwingi, makaa ya mawe, Gas, pamoja na Uranium, sasa sioni ni kwanini nchi kama Tanzania kushindwa ku-utilise hizi resources tulizo nazo ili kuwezesha Tanzania na Watanzania kupata ufumbuzi wa Umeme wa kudumu na kuzidisha chachu ya maendeleo nchini Tanzania!? Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) mnafanya kazi gani na kushindwa kuwekeza millions of money ktk hizi Nyanja na kupata ufumbuzi wa tatizo la umeme Tanzania?? Mnashindwa ata kwenda kukopa nje au kushirikiana ku-invest pamoja na makampuni mengine ktk hizo nyanja?? Serikali mpo wapi mnashindwa kwenda kukopa nje ya nchi ili kuondoa tatizo la umeme Tanzania?? Tusidanganyane kwamba mnataka maendeleo nchini Tanzania kama mnashindwa ku-sort out ili tatizo la umeme once and for all!!?? Nendeni kakopeni ktk institutions mbalimbali duniani na wapeni tenders watu walio serious watupatia solutions, mbona tunashindwa na nchi mbalimbali za Africa ambazo hazina matatizo kama sisi?? Kwanini Tanzania!!!!
Naipenda nchi yangu sana, napenda maendeleo ya nchi yangu sana lakini mwenendo tulio nao unanisikitisha sana tena sana, vijana wengi hawana kazi, vijana wengi hawana pesa, wananchi wengi hawana elimu, nchi haina maendeleo, na umeme pia mnawakatia hawa hawa wananchi na kushindwa kuwapa ufumbuzi wa kudumu, je mnaipeleka nchi hii kwenda wapi??? Hakuna uzalishaji bila umeme, hakuna maendeleo bila ya uzalishaji, hivyo kwa yoyote anayehusika ktk ngazi za juu usomapo ujumbe huu ningeomba mtafute ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la umeme nchini Tanzania ili kuzidisha maendeleo, uzalishaji, ukuaji wa uchumi, idadi ya wawekezaji kuongezeka na pia kuleta mwanga ndani ya watanzania waliokosa kila kitu.
Pia wewe mtanzania, ningeomba uweze kuongea na mwakilisha wako wa sehemu unayokaa haswa haswa wabunge wenu ili waweze kuwapigania na kuwatetea haki zenu ndani ya bunge na kuwezesha kupata ufumbuzi wa shida hii kubwa iliyokaa miaka 49!! Na kama ikiwezekana wahusika wawajibishwe maana sijawahi kuona Tanzania wahusika wanawajibishwa! Na kama wewe ni mbunge basi peleka hoja hii bungeni ili badala ya serikali kununua majenereta, watafute serious long term solutions!
Nawaomba mtoe comment zenu nyingi sana kwa uhuru maana nina uhakika wahusika wengi watasoma hii post ili nao wasikie kilio chenu.
Naomba niishie hapa maana nina uchungu mwingi kwa uzembe wa watu wachache wanao fanya raia zaidi ya Milioni 40 kuteseka kwa ili tatizo la umeme. Nilitaka kusahau, Sinza hatuna umeme wa kudumu zaidi ya wiki nzima!! Tanesco wanakata umeme kila dakika na kurudisha kila dakika watakavyo bila ya kujali kuungua kwa mamilioni ya gharama za vitu ambavyo wateja wao wanavyo.
Nashukuru.
Mtanzania
No comments:
Post a Comment