Monday, July 20, 2009


Makocha waangalie wazawa zaidi - Mgosi
Mussa Hassan Mgosi mshambuliaji wa timu ya soka ya Simba amesema licha ya changamoto iliyopo sasa katika soka la Tanzania kutokana na kuwa na wachezaji wengi wa kigeni, amewataka makocha kutoa kipaumbele zaidi kwa wachezaji wazawa. Mshambuliaji huyo wa Simba anayekwenda Norway kuungana na Henry Joseph, alisema si jambo jema kwa makocha kupapatikia wachezaji kutoka nje ya nchi na hasa wenye viwango vidogo. "Makocha waangalie sana wachezaji wazawa, si...
Mussa Hassan Mgosi mshambuliaji wa timu ya soka ya Simba amesema licha ya changamoto iliyopo sasa katika soka la Tanzania kutokana na kuwa na wachezaji wengi wa kigeni, amewataka makocha kutoa kipaumbele zaidi kwa wachezaji wazawa. 

Mshambuliaji huyo wa Simba anayekwenda Norway kuungana na Henry Joseph, alisema si jambo jema kwa makocha kupapatikia wachezaji kutoka nje ya nchi na hasa wenye viwango vidogo. 

“Makocha waangalie sana wachezaji wazawa, si kwa sababu ni mchezaji wa kulipwa kutoka nje amesajiliwa basi atacheza tu hata kama hana kiwango kumzidi mchezaji wa hapa nyumbani,” alisema. 

“Tunajua kuwa kuja kwa wachezaji wa kigeni ni changamoto kubwa kwetu katika ligi yetu, lakini usawa uangaliwe zaidi, kuna wachezaji wa hapa nchini ni wazuri kuliko wa kigeni, lakini hawapewi nafasi, kwa sababu tu kuna wachezaji kutoka nje,” alisema Mgosi. 

“Mfano ligi ya msimu uliopita kulikuwa na wachezaji wengi tu wa kigeni, lakini baadhi yao tu ndio waliofanya vizuri ila wengi wao hatukuona mchango wao katika timu, na badala yake wachezaji wa hapa nchini wengi ndio waling’ara,” alisema Mgosi. 

Alisema pia wachezaji wazawa itabidi wajitume ipasavyo kukabiliana na changamoto hiyo kama kweli wana nia ya kupata namba katika kikosi cha kwanza. 

No comments:

Post a Comment