Monday, August 16, 2010



Hapa ndio mlango wa kuingilia,ambapo kiingilio kilikuwa ni sh.500 kwa mkubwa na 300 kwa mwanafunzi.Kusema ukweli ingawa waweza kuona ni kiasi kidogo sana hicho lakini nilishuhudia wanafunzi wengi wakirudi mana walishindwa kuingia kwa sababu ya kiingilio kuwa kukubwa sana ukulinganishwa na miaka iliyopita.



Tulipita  banada lililokuwa lina husika na mazao kama mihogo,mahindi,mtama mazao mengine ya nafaka.

Hii ni mashine ambao inatumika kuongeza thamani zao la muhogo.


Mtaalamu wa zao la mihogo akitupa mawili matatu ya  namna ya kugundua magonjwa ya zao la muhogo.

Ni upandaji wa mbegu za mazao kama muhogo na migomba kwa njia ya chupa

Wenzetu hua wanakuja kupata utaalamu.


Wakulima wanapaswa kuiangalia baiskeli kwa jicho la tatu mana niliyoyakuta huku nilipigwa na bumbuwazi.
Hii baiskeli inatumika kupukuchulia mahindi na pia unaweza kuchaji simu ya aina yeyote.Usishangae ndio ukweli,usijiulize sana subiri nikuonyeshe!

Upande huu ni kwa ajiri ya kupukuchulia mahindi tu

Hapa ndio kicharge simu

Angalia vizuri juu ya kiti cha nyuma unaiona simu ikiwa inachajiwa?


Nikaingia banda la sokoine napo nilifurahia kitu kimoja tu.Ingawa kuna mengi yaliniacha mdomo wazi kama hili la mbuzi hapo chini

Wadau angalia jinsi uchafuzi wa nmazingira unavyowaathiri wanyama.Mbuzi huyu alikula mifuko ya naylon

Natumai sasa unaiona vizuri zaidi

Guess what!hapa palinifurahisha sana mana nikakuta  togwa lililowekwa vizuri na katika mazingira ya kibiashara.Kama kawa mzaramo halisi hili huwa halimpiti ikabidi nilishughikie.Natumai mambo mazuri kama haya tuyaone katika maduka yetu wakati ndio huu.


Hii picha imetengenezwa kwa kutumia majani ya mgomba


Aliyefanya hii shughuli yote ni kaka chiga nipo nae kwenye picha hapo.Jamaa aliniambia walitengeneza picha ya mh.Jakaya kikwete lakini hata haikukaa sana watu wanaojua sanaa waliinunua kwa bei ya juu sana.
Ukitaka akutengenezee picha yako kama hivyo wasiliana nae kwa namba 0713436828.

Nilipenda maandishi ya tshirt yake imebidi niwawekee myaone


Sanaa zingine wanazotengeneza ni zile zinazohusika na zao la minazi kama unavyoona hapo juu



No comments:

Post a Comment