Wednesday, June 10, 2009



Serengeti Boys timu ya vijana ya Tanzania U - 17 wikiendi hii ilitoa onyo kali kwa wapinzani wake kwenye michuano ya Afrika Copa Coca - Cola kwa kuisambaratisha Ethiopia 5 - 0 katika mchezo wa ufunguzi uliochezwa kwenye uwanja wa Absa mjini Pretoria jana.

Mchezaji Joseph Mahundi alifungua kalamu hiyo kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 9 kabla ya Himid Mkami kufunga bao la pili dakika 33.

Tanzania ilifanya shambulizi lingine la nguvu dakika tano kabla ya mapunziko na kupata bao lake la tatu kupitia Issa Rashid.

Ethiopia walionekana kubadilika kipindi cha pili, lakini walijikuta wakishia kupokea kipigo kwa kufungwa bao la nne na Murshid Rashid dakika ya 51.

Ikicheza kwa kujiamini na kupigia pasi fupi fupi Serengeti Boy ilikamilisha karamu yake kwa kufunga bao la tano dakika 63 kupitia Mohamed Marzuki.

Kocha wa Tanzania, Rodrigo Stockler alisema ushindi huo mkubwa ni mafanikio makubwa kwake na ishara nzuri kwa wachezaji wake kufutwa mafundisho yake.

No comments:

Post a Comment