Friday, October 29, 2010

Tupime-tujue club
THOMSON.M.SANGA,(Muasisi na mlezi tupime-tujue club)
Thomson sanga “vijana tunachangamoto nyingi sana katika uliwengu wa sasa na inatubidi tuwe waangalifu ili kuweza kukabili-ana nazo.Kuna magonjwa mengi na vishawishi vingi ambavyo vinachochea katika kuturudisha nyu-ma kielimu na kimaisha.
Wakati wa kumtegemea mtu mwingine asimame badala yetu umekwisha na hatunabudi kuungana kwa pamoja ili kuzikabili changamoto hizi.

Shule ya sekondari lugoba imenipa mwangaza katika kuweza ku-shirikiana na vijana wenzangu ili kutafuta mbinu mbali tunazoweza kuzitumia katika kukabiliana na changamoto zinazotukabili sisi vijana kwa ujumla.
Naomba wewe kijana na jamii kwa ujumla tutambue kuwa UKIMWI ni changamoto namba moja ambayo tun-atakiwa kuikabili bila kukata tama a na kurudi nyuma.

Mimba za utotoni ni jambo ambalo hatuna budi kulipiga vita kwani huyu kijana anayeharibiwa maisha yake leo ni hasara kwa taifa la leo na kesho pia”
Binafsi naamini “vijana bila ukimwi inawezekana”na “vijana tunaweza endapo tutapewa nafasi”.

MAHALI TULIPO.

Tupime-tujue club tupo kilomita 23 pembezoni mwa barabara iendayo tanga kutoka chalinze.Tupo shule ya sekondari lugoba
          
“Vijana tuna nafasi kubwa ya kuhakikisha tunaweza kujilinda na kuepuka vishawishi na vikwazo vinavyoweza kutukwamisha katika kutimiza ndoto zetu za kuwa wanasheria, walimu,mainjinia,madaktari n.k.

Wengi wetu tumezoea mfumo wa kusubiri kusemewa na watu wengine kama wazee,wazazi na walimu.Wakati umefika sasa kwa sisi kuweza kujitambua na kujilinda na vikwazo na mazingira ya ulimwengu huu wa sasa wa sayansi na teknolojia.Kwa kushirikiana tunaweza na kwa msaada wa jamii zetu tunaweza kufanikiwa zaidi.
Tusisubiri kila kitu kusemewa na watu wengine kwani uwezo tunao,nia tunayo na sababu pia tunazo.Tuamke sasa!!!”
“Vijana wa wakati huu ni tofauti na vijana wa zamani,sayansi na teknolojia ya karne hii pamoja na utandawazi vinachangia kutufanya tubadilike.Pamoja na haya yote ni jukumu letu wenyewe kujilinda na kujiweka katika hali ya usalama ili kulinda mila na desturi za nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa magonjwa sio sababu ya kufanya ndoto zetu zisitimie”

MELKIORY JOHNBOSCO;
(Mwenyekiti 2008-9)

No comments:

Post a Comment